Mbinu za kienyeji za kusindika asali zinahusisha hatua kadhaa ili kuhakikisha mavuno bora. Tenganisha asali na masega baada ya kuvuna, huku ukiweka uwiano sahihi wa asali iliyoiva na ambayo haijaiva.
Kuanza mchakato, andaa zana muhimu amabazo ni pamoja na: chujio, uma ama kisu, na kifaa maalum cha kuchimba asali. Weka kwenye masega kwenye chujio ili kutenganisha asali na masega. Kuna njia mbili za kufanya mchakato huo.
Kwanza, ukitumia chujio ambapo masega hukatwa katika vipande vidogo. Panga vipande vya masega kwenye chujio na uanze kuviponda kwa kutumia kisu au uma. Unapoponda masega, hakikisha kwamba mtungi au chombo kimewekwa chini ya chujio ili kukusanya asali. Ni muhimu kujua kwamba njia hii inaweza kuchukua muda mwingi.
Mbinu mbadala
Vinginevyo, unaweza kutumia kifaa maalum cha kuchimba asali. Anza kwa kukata masega katika vipande vidogo kwa kutumia uma au kisu na kuviweka kwenye kifaa cha kuchimba asali. Endelea kuongeza vipande vya masega ndani ya kifaahadi kitakapojaa. Kisha bonyeza masega ukitumia shinikizo la kifaa ili kondoa asali yote. Ili kuhakikisha kwa asali yote inatolewa kwenye masega, shinikiza masega hadi usiku kucha, na mwisho utasalia na nta tu.
Kwa kufuata mbinu hizi za kienyeji za kusindika asali, unaweza kutenganisha asali na masega kwa ufanisi, na hivyo kuruhusu uvunaji bora wa asali.