Matunda ya karakara ni mmea wa kutambaa. Matunda yaliyokuzwa vizuri hutolea wakulima pesa kutokana na soko tayari kwa mwaka mzima. Kusimamisha na kupogoa matunda husababisha mavuno mazuri.
Matunda ya karakara yana hatua rahisi ya ukuaji. Tawi kuu hutoa matawi ya pili na ya tatu. Matawi ya pili hutoa matunda zaidi, lakini kwa uzalishaji bora usiruhusu matawi ya pili kujiunge na tawi mkuu. Pia hakikisha kwamba sehemu zote za mmea zinapata mzunguko wa hewa wa kutosha ili kutoa maua vyema. Kupogoa matawi ya pili huhimiza kutoa matunda zaidi, na hivyo mapato zaidi.
Kusimamisha matunda
Simika vigingi kwa umbali wa mita 3 katika safu, na mita 3–6 kati ya safu. Funga waya katika kila safu mita 2 kutoka ardhini. Panda miche kwa muachano wa mita 6 katika safu. Simamisha mimea wakati ina urefu wa mita 1, na ruhusu tawi moja kwa kila kamba au waya.
Kupogoa
Pogoa matawi yote ya pili hadi tawi kuu litakapofika kwenye waya. Vile vile, vunja tumba la juu mara tu linapofikia waya ili kuwezesha matawi mengine ya pembeni kukua. Ruhusu matawi kuu mawili pekee yakue katika mwelekeo tofauti kwa waya. Matawi ya pili hutoa matunda. Kupata mavuno mengi, pogoa vizuri kwa sababu kunachochea uzalishaji wa matunda. Pia, pogoa matawi ya tatu ili yasijiunge na tawi kuu pamoja na matawi ya pili. Daima ondoa matawa ya pili matatu ambayo yamekomaa sana baada ya kuvuna. Ondoa sehemu za mmea zilizokufa, na majani magonjwa pamoja na ya manjano.