»Kushughulikia vitunguu kabla na baada ya kuvuna«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=0uJvYE8eFqo

Muda: 

00:07:17
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Osman Dawda

Wakulima wanapaswa kuvuna vitunguu kwa uangalifu ili kudumisha na kuimarisha ubora wavyo. Ubora wa vitunguu unapopungua, bei ya sokoni pia hupungua.

Ni muhimu sana kutambua ishara za ukomavu sahihi na kuvuna katika wakati sahihi. Ishara hizi ni pamoja na vituungu huanza kuonekana juu ya ardhi, udongo ulio karibu na mmea hupasuka, ncha za majani hukauka, majani huanza kunyauka na kudondoka. Uvunaji hufanywa ama kwa mauzo ya mara moja (siku 70 hadi 80 baada ya kupandikiza) wakati ukubwa wa vitunguu ni gramu 70 hadi 90 au kwa kuhifadhi. Huku kunafanywa kutokana na bei ya chini iliyo soko, na kutunza ugavi wa vitunguu sokoni.

Mchakato wa kuvuna

Vitunguu bora vinapaswa kuwa na uimara mzuri, ngozi ya nyama iliyoshikamana, saizi na rangi inayofaa, harufu nzuri, bila uharibifu wowote. Uvunaji unaweza kufanywa kwa kutumia mikono au majembe madogo. Uvunaji wa mapema hufanywa kwa kutumia mikono wakati majani bado ni mabichi au yamekauka kiasi. Uvunaji wa kuchelewa hufanywa kwa kutumia majembe madogo wakati majani yamekauka. Baada ya kuvuna, kusanyia vitunguu chini ya kivuli na vitandaze ili kuepuka ongezeko la joto.

Kisha kata majani kwenye eneo la shingo huku ukiacha cm 1–2 ili kuzuia maambukizo na kuepuka kukauka kupita kiasi.

Mbinu za usimamizi baada ya mavuno

Kwanza sitisha kumwagilia ili kusaidia kuunda majani magumu ambayo hupunguza upotevu wa maji kutoka kwa majani ya ndani. Kisha hifadhi vitunguu chini ya kivuli kati ya nyuzi 27 – 30 kwa muda wa siku 5 hadi 10 ili kurefusha maisha ya vitunguu vilivyovunwa. Hata hivyo, epuka kuvikanyaga, kuvipakia kupita kiasi ili kuepuka uharibifu.

Pili, shughulikia na fungasha vitunguu kwa uangalifu ili kupunguza uharibifu. Safirisha vitunguu ukutumia vyombo vikubwa. Wakati wa kuhifadhi, ondoa nyezo zisizofaa na vitunguu vilivyoharibika. Ainisha vitunguu, na kisha vihifadhi kwenye jukwaa lililoinuliwa katika chumba kikavu ambacho kinaingiza hewa vizuri, huku ukizingatia usafi chumbani. Hakikisha paa halivuji, na pia fuatilia pamoja na kuondoa vitunguu vilivyooza na vilivyoshambuliwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:28Ni muhimu sana kutambua ishara za ukomavu sahihi na kuvuna katika wakati sahihi
01:2901:52Vitunguu huvunwa na kuhifadhiwa kwa sababu mbalimbali, sitisha kumwagilia maji.
01:5302:39Vuna mapema wakati majani yanaponyauka huku ukitumia mkono au jembe.
02:4003:34Vuna na kusanyia vitunguu chini ya kivuli, vitandaze, kata majani kwenye eneo la shingo la kitunguu.
03:3504:34Hakikisha hatua za kabla ya kuvuna zinachukuliwa, na uangalie sifa za vitunguu vilivyokomaa.
04:3505:05Vuna vitunguu visivyo na kasoro wala uharibifu wadudu, sitisha kumwagilia siku 5 hadi 10.
05:0605:29Kisha hifadhi vitunguu chini ya kivuli kati ya nyuzi 27 – 30 kwa muda wa siku 5 hadi 10. Hata hivyo, epuka kuvikanyaga, na kuvipakia kupita kiasi.
05:3005:51Shughulikia, fungasha na safirisha vitunguu kwa uangalifu.
05:5206:18Usafiri kwa kutumia magari yaliyoboreshwa, ondoa vitunguu vilivyoharibika.
06:1906:38Ainisha vitunguu , vihifadhi kwenye jukwaa lililoinuliwa na vitandaze chumbani.
06:3906:56Hakikisha chumba cha kuhifadhia kinapenyeza hewa vizuri. Chambua vitunguu vilivyoharibika. Epuka uvujaji wa paa.
06:5707:08Chunguza vitunguu katika chumba cha kuhifadhia kila wiki au kila mwezi, na ondoa vitunguu vilivyoshambuliwa, chunguza soko na uondoe vitunguu vya ubora duni.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *