Kushughulikia chanjo; Kipimo na matumizi kwa ng‘ombe wa maziwa

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ZLJ1cNqCfWI

Muda: 

00:04:50
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Boehringer Ingelheim Cattle Health

Kwa kuwa ni mojawapo ya mambo yanayoathiri ufugaji wa wanyama, afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana.

Ufanisi wa chanjo hutegemea uwezo wa mnyama wa kuitikia chanjo, utunzaji sahihi na jinsi ya kutoa chanjo. Chanjo huhifadhiwa kwenye chupa kulingana na kipimo kinachohitajika.

Kudunga mnyama chanjo

Chanjo hutumika moja kwa moja bila kuichanganya, na katika hali hii unapaswa kuilinda dhidi ya joto, mwanga wa jua pamoja na baridi kali inapohifadhiwa. Hifadhi chanjo kwenye jokofu iliyo kati ya nyuzi joto 35 hadi 40. Pia hifadhi bomba la sindano kwenye jokofu ambayo huzuia mwanga wa jua kuingia, pamoja na kulinda chanjo dhidi ya joto kali.

Vile vile, epuka kuchanja wakati ng‘ombe hajakauka au mchafu. Kabla ya kutumia chanjo, tikisa kwa upole au viringisha chupa ili kuichanganya ipaswavyo. Shikilia bomba ya sindano na chupa kwa mkono mmoja na tumia mkono mwingine kuondoa kipimo cha chanjo unachohitaji. Kisha chomoa sindano kwenye chupa huku ukielekeza juu, na uondoe hewa kwenye bomba la sindano.

Kabla ya kutoa chanjo kwa mnyama, mfunge na kisha uelekeze sindano mahali sahihi. Hakikisha eneo hilo ni safi.

Kwa sindano ya chini ya ngozi, tumia sindano mpya. Baada ya kubaini sehemu sahihi, vuta ngozi ya shingo ya mnyama ili kuunda mahali pa kudunga sindano huku ukiepuka kuathiri msuli. Kisha ingiza chanjo, na uondoe sindano huku ukiachilia ngozi.

Baada ya kuchanja, safisha sindano na maji ya moto, walakini usitumie dawa za kuua viini. Weka lebo kwenye kila bomba la sindano ili kuonyesha kilichomo.

Hatimaye kwa matokeo bora, chanjo inapaswa kutumika mara tu inapofunguliwa, na sindano zinapaswa kutupwa ipaswavyo kwa kufuata kanuni.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:15Ufanisi wa chanjo hutegemea na uwezo wa mnyama wa kuitikia chanjo
00:1600:18Pia hutegemea utunzaji sahihi na jinsi ya kudunga chanjo.
00:01900:35Chanjo huhifadhiwa kwenye chupa kulingana na kipimo kinachohitajika
00:3600:59Chanjo aina hii hutumika moja kwa moja bila kuichanganya
01:0001:06Linda chanjo dhidi ya joto, mwanga wa jua pamoja na baridi kali
01:0701:13Hifadhi chanjo kwenye jokofu iliyo kati ya nyuzi joto 35 hadi 40.
01:1401:23Pia hifadhi bomba la sindano kwenye jokofu.
01:2401:32 Epuka kuchanja wakati ng‘ombe hajakauka au ni mchafu.
01:3301:40Kabla ya kutumia chanjo, tikisa kwa upole au viringisha chupa ili kuichanganya ipaswavyo.
01:4101:44Shikilia bomba ya sindano na chupa kwa mkono mmoja
01:4501:49Ingiza sindano kwenye chupa ili kuondoa kipimo cha chanjo unachohitaji.
01:5002:05chomoa sindano kwenye chupa huku ukielekeza juu, na uondoe hewa.
02:0602:41Funga mnyama kabla ya kumdunga chanjo
02:4202:57Tambua mahaji pa kudunga sindano, na hakikisha pasafi.
02:5803:16Kwa sindano ya chini ya ngozi, tumia sindano mpya. Vuta ngozi iliyo kwenye shingo ya ng‘ombe ili kuunda muundo wa hema
03:1703:23Ingiza sindano chini ya ngozi iliyovutwa na epuka kudunga misuli.
03:2403:37Ingiza chanjo, na uondoe sindano na kisha achilia ngozi.
03:3804:00Baada ya kuchanja, safisha sindano na maji ya moto, walakini usitumie dawa za kuua viini.
04:0104:22Kwa bomba ya sindano ambayo inaweza kutukika kutoa vipimo kadhha vya dawa, itumie kwenye bidhaa hiyo hiyo kila wakati.
04:2304:26Kwa matokeo bora, chanjo inapaswa kutumika mara tu inapofunguliwa
04:2704:33Sindano zinapaswa kutupwa ipaswavyo kwa kufuata kanuni.
04:3404:50Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *