Mpilipili huchukua miezi 3 kukomaa, na zao hilo lina soko kubwa lililo tayari na hivyo ni chanzo kikubwa cha mapato.
Unapokuza pilipili tumia pembejeo za kikaboni ili kuuza bidhaa katika soko la kimataifa. Wakati wa kuvuna, ainisha pilipili kulingana na rangi. Pilipili ina matumizi kadhaa ambayo ni pamoja na, kufanya kama kihifadhi, ni chanzo cha mapato, kiungo cha chakula, kiamsha hamu. Pilipili pia hupunguza kiwango cha kolesteroli, huzuia kisukari, huongeza vitamini C nakadhalika.
Kilimo cha pilipili
Kwanza tafuta mbegu bora na utengeneze kitalu. Baada ya hapo palilia baada ya siku 21.
Pandikiza miche baada ya mwezi 1 na nyunyuzia dawa za kikaboni ili kudhibiti wadudu na magonjwa.
Palilia mara mbili kwa wiki ili kupunguza ushindani wa virutubisho, na nyunyizia dawa ili kupata mavuno mazuri.
Ongeza mbolea ya kikaboni shambani ili kuboresha rutuba ya udongo na kupanua uzalishaji.
Panda mseto na mazao mengine ili kuongeza tija pamoja na kudhibiti magonjwa.
Panda pilipili kwa umbali wa futi 5 X 5 ili kurahisisha kunyunyizia dawa na kuvuna. Ainisha na fungasha pilipili kulingana na rangi ili kukidhi mahitaji ya walaji.