Kudumisha shamba la mikorosho pamoja na mazao ya kila mwaka husababisha mavuno mengi na mapato ya ziada. Kwani, miti ya mikorosho ni muhimu sana kijamii, kiuchumi, na kimazingira. Mikorosho hukuzwa kwa kutoa bibo/kanju na juisi.
Kusimamia shamba la mikorosho
Ondoa vichaka na magugu kabla ya kulima ili kurahisisha kilimo. Baada ya kuvuna, kata matawi yasiyotoa matunda ya korosho, na yale yanaojikunja ili kuruhushu upenyezaji mzuri wa mwangaza wa jua. Hakikisha kuna upenyezaji wa hewa ya kutosha ambayo kwamba huhitajika kwa kuota vizuri, na kutoa maua kwa mavuno mengi.
Epuka kulima katika mashamba ya mikorosho kwa kina kirefu, kwani usikate mizizi inayolisha mimea. Panda njugu au soya katika kipindi sahihi, na msongamano sahihi ili kuimarisha ardhi na nitrojeni. Hivyo hivyo, epuka kupanda pamba, mbaazi na mikunde, kwani hizi hushambuliwa na wadudu sawa na mikorosho.
Hakikisha upaliliaji sahihi na wa kawaida, ili kuongeza mzunguko wa hewa, na kupunguza ushindani wa virutubisho ili kupata mavuno zaidi. Acha mabaki ya mimea shambani wakati wa kuvuna, ili kuongeza rutuba ya udongo. Mwishowe, kukusanya bibo au korosho mara tu zinapoanguka ili kuepuka kupoteza ubora wake.