»Kulisha panya wakatanyasi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/feeding-grasscutters

Muda: 

00:09:00
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

DEDRAS , Nawaya, Songhai, Centre

Mkatanyasi ni panya mpya wa msituni anayefugwa nyumbani. Waafrika wengi hufurahiya kula nyama yake. Kufuga mkatanyasi ni shughuli nzuri ambayo huingiza mapato, kwani hauhitaji fedha nyingi kuanzisha mradi huo.

Ili kufanikiwa na ufugaji huu, andaa makazi mazuri wa wanyama, wachunguze kwa makini, na wape lishe ya usawa. Chakula chao kimsingi ni lishe ambacho ni pamoja na nyasi za kudumu kama vile panicum, pennisetum ambazo zinaweza kuvunwa kutoka porini au kulimwa. Majani ya mitende, nafaka, mashina na njugu.

Nyasi na matunda

Lishe linaweza kuongezwa na matunda ambayo hayajaiva kama vile papai na maembe. Matunda yaliyoiva yaepukwe kwa sababu husababisha kuhara na uvimbe. Miwa, mizizi ya nyasi, mihogo na viazi vikuu vilivyokatwa katika vipande vidogo pia vinaweza kuongezwa. Uangalifu unafaa kudumishwa wakati wa kuwalisha wanyama mihogo, kwani mihogo zingine zina uchungu na sumu. Zizi lazima zisafishwe. Walishe wakatanyasi kiwango cha kutosha cha lishe kila asubuhi, mchana na jioni. Mizizi na miwa inafaa kupunguzwa kwani inathiri ukuaji na meno ya wakatanyasi.

Lishe la mchanganyiko

Malishe hutayarishwa nyumbani kwa kuchanganya mahindi, mafuta, wishwa ya ngano na chumvi. Malishe haya huongezwa pamoja na vipande vidogo vya mizizi, matunda ambayo hayajaiva, na maji kwani ni rahisi kuliwa kwa mnyama.

Malishe yaliyochanganywa husaidia wakatanyasi kuzaa watoto wenye nguvu, ukuaji bora na afya. Malishe yaliyolainishwa kuwa unga husababisha magonjwa ya kupumua.

Kuvuna Lishe

Uvunaji hufanyika mchana kwa sababu umande wa asubuhi hubeba vimelea. Lishe lililovunwa huhifadhiwa kwa muda kadha kabla ya kulishwa wakatanyasi. Hii husaidia kuzuia magonjwa kama vile kuhara unaosababishwa na vimele katika lishe iliye unyevu.

Kutambua lishe lililokomaa

Lishe ambalo lina kiwango cha fumuele cha kutosha huvunwa. Panicum iliyokomaa ina maua, shina lake lina tundu ndani likikatwa. Pennisetum, huwa tayari wakati shina huanzu kuonekana.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:36Mkatanyasi ni panya mpya wa msituni anayefugwa nyumbani.
00:3700:55Kufuga mkatanyasi ni shughuli nzuri ambayo huingiza mapato
00:5601:19Haihitaji fedha nyingi kuanzisha.
01:0001:25Ili kufanikiwa na ufugaji huu, makao sahihi na lishe ya usawa inafaa kutolewa
01:2503:56Safisha makazi ya wanyama na uwatunze vizuri kwa ukuaji bora
03:5704:26Lishe linaweza kuongezwa na matunda ambayo hayajaiva
04:2705:12Aina nyingine za mihogo zina uchungu na sumu. . Epuka kuwapa wanyama wachanga lishe la majani.
05:1205:51Punguza kiwango cha miwa.
5:5205:58Meno marefu sana husababisha ugumu wa kula.
05:5906:52Malishe yaliyochanganywa husaidia wakatanyasi kuzaa watoto wenye nguvu, ukuaji bora na afya.
06:5307:07Malishe yaliyolainishwa kuwa unga husababisha magonjwa ya kupumua.
07:0807:12Wape wanyama maji ya kutosha
07:1307:17Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *