Konokono huishi katika mazingira yenye unyevu mwingi, na hukusanywa kijadi ili kuliwa. Nyama yao ni nzuri kwani imekithiri protini, madini na kalisiam kuliko nyama ya ng‘ombe hata na maini. Ni muhimu sana kwa watoto, na wanawake wajawazito au wanaonyonyesha.
Kuongezeka kwa idadi ya watu, uharibifu wa misitu na upanuzi wa kilimo hufanya ukusanyaji wao mwituni kuwa mgumu. Kwa hivyo, kuna hitaji la kilimo cha konokono. Kusimamia shamba la konokono ni rahisi kwani halihitaji rasilimali nyingi, nafasi kubwa au wakati. Kwa hivyo, kilimo hiki kinaweza kuongeza mapato kwa mkulima.
Konokono hula nyenzo za mimea kama vile majani, matunda na mizizi. Malisho ya ziada husaidia konokono kufikia 400-500 g kwa miezi 4.
Kuandaa chakula cha konokono
Vipimo 3 vya wishwa ya ngano vinachanganywa na vipimo 3 vya keki ya nazi, vipimo 3 vya makombe yaliyosagwa na kipimo 1 cha keki ya soya. Ngano hutoa nguvu, keki ya nazi hutoa nguvu na protini, makombe ya chaza hutoa kalsiamu, na keki ya soya hutoa protini.
Iwapo hakuna rasilimali ya kutosha, unaweza kuandaa lishe ukutumia wishwa ya mahindi au mchele. Keki ya njugu au unga wa samaki unaweza kutumika kama chanzo cha protini. Kalsiamu husaidia kuimarisha makombe. kombe la yai, kombe la konokono au mifupa ya wanyama inaweza kusagwa baada ya kuchomwa motoni, na kuchanganywa na lishe. Konokono hula udongo pia ambao una virutubisho na kalsiamu
Kulisha konokono
Konokono hulishwa mara moja kwa siku wakati wa jioni kwa sababu hutoka usiku tu. Wape konokoko maji ukitumia chombo kilicho na kina kifupi ili kuruhusu konokono kunywa vizuri. Eneo la kulisha linafaa pia kuwa safi.
Tahadhari: Usiwape konokono Malishe machungu kama vile mwarobaini, papai na majani ya mtukutu kwani huathiri ladha. Kuwalisha konokono lishe tamu husababisha ladha nzuri.
Kamwe, usichanganye chumvi kwenye lishe kwani chumvi hukausha maji mwilini na kuua konokono.