Maarifa juu ya ukuzaji wa vitunguu na mbinu bora za usimamizi ni muhimu katika kuongeza mavuno.
Ukuzaji wa vitunguu huanzia kwenye kitalu. Ili kutengeneza kitalu cha vitunguu, unahitaji udongo mweusi ambao ni tifutifu. Weka mboji na kuichanganya na udongo vizuri. Mboji lazima iwe imeoza kikamilifu kwa sababu mboji mbichi huchoma mbegu za vitunguu. Tawanya mbegu kwenye kitalu na ukitandaze kwa wiki moja. Baada ya wiki moja, ondo nyasi na umwagilie maji mara kwa mara. Miche ya vitunguu huwa tayari kupandikizwa wiki 4 hadi 6 baada ya kupanda
Kupandikiza na kushughulikia mimea
Wakati wa kupandikiza, panda vitunguu kwa muachano wa 10cm kati ya mimea. Vitunguu huchukua takriban miezi 4 kukomaa, lakini wiki 3 za mwisho kabla ya kuvuna huhitaji hali ya hewa isiyo na mvua.
Wadudu waharibifu wa vitunguu ni wadudu chawa, ambao ni hatari sana wakati wa kiangazi kwa sababu hutaga mayai kwenye udongo uliokauka. Umwagiliaji wa maji unaweza kupunguza asilimia kubwa ya mayai hayi. Wadudu chawa wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia kemikali, lakini unyunyizaji wa dawa bora ufanywe jioni.
Ubwiri unga ni ugonjwa hatari wa vitunguu. Unaweza kudhibitiwa kwa kutumia viuatilifu. Tumia dawa za kuzuia ukungu kabla ya ugonjwa kuibuka, pamoja na dawa za kutibu wakati ugonjwa umeshambulia mimea.