Kwa kuwa ni tunda lenye virutubisho vingi, ubora na wingi wa tikitimaji hutegemea teknolojia na mbinu za kilimo zinazotumiwa na mkulima.
Kwa kuwa ni mmea wa majani, ambao hudumu kwa mwaka, tikitimaji ni jamii ya cucurbitaceae na jina lake la kisayansi ni citrullus lanatus. Mchakato wa kupanda mmea huanza kwa kupanda mbegu kwenye vitalu, na mmea unapokua hadi urefu wa 8cm, majani makuu huanza kuonekana.
Usimamizi wa tikiti maji
Siku 10–12 baada ya kuota, jani la kwanza hukauka na kijicho huanza kuchipuka. Ili kuzuia magonjwa katika vitalu vya plastiki, bebesha au unganisha miche kwa kutumia mabua ya malenge kama njia ya kuongeza upinzani dhidi ya mnyauko wa fusari na magonjwa mengine ya ukungu yanayopatikana kwenye udongo. Muda kati ya kupanda na kupandikiza hutofautiana kutoka siku 30–40 tangu wakati wa kupanda mbegu kwenye kitalu.
Pandikiza miche kwenye udongo bila kutenganisha mizizi. Funika mzizi kwa udongo na umwagilie maji ili kustawisha mmea. Mwezi mmoja baada ya kupanda, mtikitimaji huanza kuchipuka matawi yanayotambaa na majani huanza kugawanyika.
Mwagilia mimea siku 10–12 baada ya umwagiliaji wa kwanza. Baada ya mtikitimaji kutoa majani mengi, tengeneza mitaro au matuta. Kupogoa kwa kwanza hufanywa wakati majani 4–6 halisi yanapotokea.
Vile vile, mchakato huo hurudiwa wakati matawi ya pili yanapotokea. Katika kupogoa kwa pili, ni matawi mawili tu kuu yanayoachwa. Wakati matawi haya yana majani 5–6, vijicho huodolewa ili kuruhusu uundaji wa matawi ya pili.
Funika udongo na damani ya plastiki, mboji au mchanga ili kudumisha joto la udongo na unyevu wa udongo. Wakati wa kuchanua maua, maua ya kwanza kuonekana ni ya kiume yakifuatiwa na yale ya kike ambayo hukua kutoka kwenye tawi kuu na machipukizi ya pili.
Kwa uchavushaji, vichocheo bandia huwekwa kwenye chafu ili kusababisha ukuaji wa matunda. Aina amabyo hukomaa mapema huanza kuzaa matunda kwa mwezi 1.5 na kwa miezi 2, mabua yatakuwa na urefu wa mita 1. Kutoka wakati huu mmea huwa unahitaji joto la muda mrefu.
Hatimaye, siku ya kuvunia hutegemea aina iliyopandwa, eneo, wakati wa kupandia na mfumo wa kilimo uliotekelezwa. Wakati mzuri wa kuvunia ni asubuhi.