Kuku wa kienyeji ni kitamu, na kuwakuza huchangia katika usalama wa chakula kwa vile wana gharama ndogo za kuanzisha, huhitaji ardhi kidogo, kazi kidogo, na huhitajika sana.
Changamoto kwa wafugaji wa kuku ni; soko la kuuzia, usambazaji duni wa bidhaa, kutopata huduma za ugani, vifo vingi, gharama kubwa za ulishaji na ufugaji duni.
Inashauriwa kwa wakulima kufuga kuku wengi kwa mapato mengi, na kinyesi chao kutumika kama mbolea.
Uzalishaji na uuzaji
Wakati wa kuuza kuku, pima uzani wa ndege ili kuongeza uuzaji na uzalishaji wa pamoja. Pia jenga vyumba bora vya kuku ili kuwalinda dhidi ya wanyama, wezi na hali mbaya ya hewa.
Hakikisha kuna uingizaji wa hewa katika banda la kuku huku upande mmoja ukiwa na nyavu ili kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa. Weka pumba ya mbao kwenye sakafu ili kuondoa unyevu. Tumia mfumo wa nyavu zilizoinuliwa ili kufuga idadi kubwa ya kuku na kukusanya kinyesi kwa urahisi.
Dumisha usafi sahihi na chanja siku 3 – 5 baada ya mayai kuanguliwa ili kudhibiti na kupunguza magonjwa ya virusi. Pata mafunzo juu ya chanjo na hatua za kudhibiti vimelea ili kudhibiti hasara zinazotokana na magonjwa na wadudu, pamoja na kufuata mpango wa chanjo.
Chunguza kuku mara kwa mara ili kuona vimelea kwa vile kuku wanaofugwa nje hushambuliwa sana. Nyunyiza dawa kwenye kivuli, viota, na nyufa ili kuua vimelea. Weka majani ya mitishamba kwenye maji ya kunywa ili kutibu kuku. Wape kuku chakula cha kutosha kwa ukuaji bora.