Muhogo hukua kwa urahisi unapolimwa kwenye udongo duni. Kuna njia kadhaa za kuboresha uzalishaji wa muhogo na kurudisha rutuba ya udongo.
Muhogo hustahimili ukame na una wanga(starch) zaidi, lakini protini kidogo. Manufaa na Wanga ya muhogo hupungua wakati unapovunwa mapema.
Ukuaji wa muhogo
Mizizi ya nyuzi hukua baada ya kupanda, ili kuwezesha ufyonzaji wa maji na virutubisho. Majani hutoka kwenye nundu ili yawezeshe mwangaza wa jua kufikia mmea. Katika wiki 2–3 mizizi huanza kuvimba, na wanga mwingi wa muhogo hupatikana kati ya miezi 8–12.
Kuboresha uzalishaji
Panda aina za muhogo ambazo zinastahimili na ni sugu dhidi ya magonjwa, ukame, na pia zinazoweza kutoa mavuno mengi ili kuongeza mapato. Tumia mboji au mbolea oza ili mimea iweze kunawiri zaidi.
Hali kadhalika, weka na kisha funika kipimo kidogo cha mbolea za madini ili kuboresha rutuba ya udongo. Pia, waweza kupanda mimea na jamii ya kunde kwa kuboresha rutuba ya udongo na kudhibiti magugu. Mwishowe, rekebisha mtindo wa upandaji ili kupanua mapato na kuwezesha ukuaji mzuri wa mimea.