Kukaushia mpunga juani

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=PcRxWvBJJsw

Muda: 

00:05:58
Imetengenezwa ndani: 
2013

Imetayarishwa na: 

International Rice Research Institute
Kukaushia kwa jua ni nbinu ya kienyeji ya kukausha mpunga ambayo huhitaji uwekezaji mdogo na haiathiri mazingira.
Vipima joto na vipima unyevu vinaweza kutumika kupima joto na unyevu wa nafaka mtawalia. Kukaushia nafaka kwa jua kuna faida kadhaa kwamba; ni nafuu, hakuathiri mazingira, wala hakusababishi uchafuzi wa mazingira.

Mchakato wa kukaushia mpunga kwenye jua

Tandaza nafaka juu ya sehemu ya kukaushia katika mahali  penye hewa nzuri huku ukichanganya nafaka kila baada ya dakika 30 ili ziweze kukauka haraka. Angalia halijoto ya nafaka na unyevunyevu kwa kufunika mpunga ikiwa halijoto ni zaidi ya nyuzi joto 50.
Kusanya nafaka ikiwa mvua itanyesha na pia usiku ili kuzuia nafaka kunyonya unyevu na kupasuka. Punguza unyevu hadi 18% kwenye safu ya nafaka ya nje ili kurahisisha uhifadhi kwa wiki 2 kabla ya kutumia mfumo mwingine wa kukausha. Mwishowe, kila wakati zuia wanyama kufikia nafaka, na epuka kukaushia kwenye barabara kwani huku kunaweza kusababisha uchafuzi wa nafaka.

Mapungufu ya kukaushia juani

Kukaushia juani huchelewesha mchakato wa mbegu kukauka. Na pia haiwezekani kukausha nafaka wakati wa mvua au usiku, jambo ambalo husababisha ukuaji wa ukungu. Pia ni ngumu kudhibiti halijoto kwajoto kali hupunguza ubora wa nafaka.

Mbinu za kukaushia juani

Kukaushia shambani; huku kunafanywa kwa kuweka mimea iliyokatwa juu ya ardhi au kwenye kininginizio, kwa vile nafaka zinaweza kupata unyevu usiku, ubora wazo huwa duni.
Kukausha gunzi; huku kunafanywa kwa kuweka gunzi zilizofungwa pamoja kwenye mikeka, sakaf au jukwaa, hata hivyo gunzi hukauka polepole.
Kutumia wavu au mikeka kukausha; huku hutekelezwa na wakulima wadogo kwa kuweka nafaka kwenye wavu na mikeka. Hata hivyo, gharama za kununua wavu na mikeka ni ghali, pamoja na changamoto la uchafuzi kutoka ardhini.
Kukaushia sakafuni; huku hutekelezwa na wakulima wakubwa kwa kutandaza nafaka kwenye sakafu, hata hivyo ni kazi ngumu zaidi ambayo pia huhusisha uchafuzi.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:41Kukaushia kwa jua ni nbinu ya kienyeji ya kukausha mpunga ambayo huhitaji uwekezaji mdogo na haiathiri mazingira.
00:4200:59Kukaushia nafaka kwa jua hakuathiri mazingira, wala hakusababishi uchafuzi wa mazingira.
01:0001:06 Mchakato wa kukaushia mpunga kwenye jua.
01:0701:25Tandaza nafaka juu ya sehemu ya kukaushia katika mahali penye hewa nzuri huku ukichanganya nafaka kila baada ya dakika 30
01:2601:42Angalia halijoto ya nafaka na unyevunyevu kwa kufunika mpunga ikiwa halijoto ni zaidi ya nyuzi joto 50.
01:4301:57Kusanya nafaka ikiwa mvua itanyesha na pia usiku
01:5802:16 Punguza unyevu hadi 18% kwenye safu ya nafaka ya nje ili kurahisisha uhifadhi.
02:1702:28Zuia wanyama kufikia nafaka, na epuka kukaushia kwenye barabara
02:2902:37 Mapungufu ya kukausha jua.
02:3803:04Kukaushia juani huchelewesha mchakato wa mbegu kukauka. Na pia haiwezekani kukausha nafaka wakati wa mvua au usiku
03:0505:32Mbinu za kukaushia juani
05:3305:58wasifu

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *