Pilipili ni chanzo kizuri cha mapato kwa wakulima kwa muda mfupi. Jifunze jinsi ya kuvuna, kukausha, kuchambua na kuhifadhi pilipili ili Kupunguza hasara na kuongeza fedha.
Vuna pilipili zilizoiva tu, ikiwa ambazo hazijaiva zimevunwa, zichambue. Ni bora kuvuna pilipili nyakati za jua. Pilipili huasha mikono unapovuna, kwani ni bora kutumia glavu, au kuosha mikono na sabuni au jivu, na kutumia limao.
Kukausha vizuri
Tandaza pilipili kwenye mkeka safi chini ya jua na kuzigeuza ili zikauke vizuri. Walakini, usikaushie kwenye mawe, paa ya mabati, damani ya plastiki kwani maeneo haya yana joto sana.
Tumia rafu/ shubaka la mbao au magogo kisha uweke mkeka juu yake ili kuzuia unyevu kutoka kwenye udongo kufikia pilipili. Tandaza na kugeuza pilipili kila saa ili zote zikauke kwa usawa. Pilipili zisipokauka kabisa mchana, ziache juu ya mkeka usiku kucha. Usizihifadhi kwenye mifuko ili uepuke kuchanganya pilipili zilizokauka na zile ambazo hazikukauka vizuri.
Kuainisha pilipili
Safisha mkeka, ikaushe, na iweke kwenye mawe baada ya kuitumia. Ainisha pilipili kwa kuzingatia vigezo vitatu; kwa kuondoa chembechembe na mabaki yoyote yasiyo pilipili, kuondoa zilizovunjika na ambazo hazijaiva kabisa, na zile zilizoiva kabisa. kisha tunaweza kuzihifadhi.
Epuka kuhifadhi pilipili kwenye mifuko ya plastiki ili kuzuia unyevu kufanyika ndani. Hifadhi pilipili katika magunia ya mkonge na uyaweke mahali pakavu kwenye kivuli na hewa ya kutosha. Hakikisha kwamba paa halivuji wakati wa mvua. Weka mbao chini ya magunia ili kuzuia unyevu kutoka.