Biashara ya mitende hukabiliwa na changamoto kali zinazosababishwa na fukusi mwekundu wa mitende. Fukusi wanaweza kudhibitiwa kwa kutumia njia ya kijadi ya mrija na bomba linalotumia shinikizo, pamoja na dawa inayopendekezwa.
Fukusi mwekundu akishambulia mti, huingia ndani ya shina na kudhoofisha mtende na hivyo kusababisha matunda duni. Dalili ya kwanza ya shambulio lake ni uwepo wa kiota hai kwenye shina ambacho husababisha kinyesi cha hudhurungi kinachonukia na hutiririka kupitia shimo la kuingilia kiota. Dalili nyingine ni kuona kitu kinachofanana machujo au pumba la mbao kwenye shina.
Njia za kudhibiti fukusi
Unaweza kuzuia shambulio la fukusi mwekundu kwenye mitende kwa kuwanyunyizia sulfuri au majivu, pamoja na viuatilifu. Haya huwafukuza fukusi.
Fukusi wanaweza kudhibitiwa pia kwa kutumia njia ya kijadi ya mrija na bomba, pamoja na dawa inayopendekezwa. Walakini, daima vaa vifaa vya kinga wakati wa kutumia dawa za kuua wadudu.
Ukiwa unatumia njia ya mrija, chimba mashimo 4 yawe 5cm hadi 10cm juu ya shimo la kiota, kwenye pembe ambayo itawezesha mtiririko wa dawa kuingia kwenye shina. Changanya dawa iliyopendekezwa kwa kipimo kilichopendekezwa na uimimine kwenye shina ukitumia chupa. Changamoto kubwa kwa njia hii ni kwamba wakati wingine dawa kidogo hufikia kiota kuua mabuu wa wadudu.
Bomba la moja kwa moja
Ili kutumia bomba la mashine, tambua mahali ambapo kiota kimejengwa, na uchimbe mashimo kwa cm 15 hadi 20 juu ya eneo la kiota. Unganisha kifaa cha kuchimbua kwa bomba. Jaza tanki na dawa ya kutosha na kisha uipige ndani ya shina la mti.
Baada ya kupiga dawa, funika mashimo madogo na uweka alama kwenye miti iliyotibiwa, kisha ufuatilie kwa muda wa miezi 3.
Kwa miti iliyo na uvamizi mkubwa, uharibifu unaweza kuwa usioweza kurekebishwa, na hata dawa ya wadudu haitafanya vizuri. Unachohitajika kufanya ni kukata na kuchoma au kuzika shina.