Mchele uliotokoswa au uliotiwa jota huna manufaa nyingi. Ni safi, rahisi kupikwa na una rutubishi na haivunja. Zaidi ya hayo, ni rahisi kusaga na kuuza kwa bei nzuri.
Mchele uliotiwa joto huloweshwa ndani ya maji moto, na kwenye mvuke baadaye. Lakini mchele uliotiwa haufai kuchemshwa, kwa sababu unaweza kuiva.
Jinsi ya kutengeneza
Kwa kutengeneza mchele uliotiwa moto unahitaji jiko, sufuria, chombo cha kutokosa, maji safi, kuni, turubai, kikapu, na mpunga.
Ondoa mawe yoyote, nafaka chanaga, vumbi, takataka na uchafu mwingine. Kisha weka mpunga katika chombo kilichojazwa na maji baridi. Osha na ukoroge mpunga ili chembechembe nyepesi ziweze kulea juu ya maji, kisha uziondoe. Ondoa maji na kisha uoshe mpunga tena, hadi kusiwe na vitu vyovyote vinavyoelea. Sasa, toa nusu ya maji. Ondoa mpunga kutoka kwenye chombo, na hakikisha hujachukua mawe na takataka.
Weka mpunga kwenye sufuria iliyo na maji baridi na uwasha moto. Koroga mara kwa mara. Maji yakigeuka moto kugusa, ondoa sufuria kutoka kwenye moto. Acha mpunga upoe usiku kucha. Asubuhi inayofuata ondoa vitu vyovyote vinavyoelea juu ya maji. Ondoa mpunga kutoka kwenye chombo na uumwage ndani ya kikapu.
Sasa unaendelea na kutumia chombo cha kutokosa. Weka sufuria kwa moto na uongeze maji kiasi. Kisha weka chombo cha kutokosa juu ya sufuria. Ni muhimu kwamba sehemu ya chini ya chombo hiki iwe mbali na maji, kwa sababu mpunga utaanza kuiva. Weka mpunga ndani ya chombo hiki. Sasa acha nafasi kidogo juu ya mpunga ili uweze kuvimba. Funika mpunga kwa kutumia gunia, kisha funika na kifuniko maalum. Ziba kabisa nafasi kati ya sufuria na chombo cha kutia joto/kutokosa kwa kutumia kitambaa safi, ili kuzuia kupoteza mvuke. Baada ya dakika 30 mpunga huwa tayari na maganda mengi yamefunguka.
Kausha mpunga kwenye mahali safi kama turubai. Usikaushe mpunga kwa jua kwa muda mrefu, na uiweke kwenye kivuli baada ya muda. Unafaa kupindua mpunga mara kwa mara.