Faida za kilimo mseto kwa mimea ya kudumu ni nyingi. Eneo lile lile la ardhi lenye mimea michache ya kahawa au kakao linaweza kutoa mavuno kidogo lakini linaweza fidiliwa na mavuno ya mazao ya mengeni yaliyopandwa.
Mifumo ya kilimo mseto inaweza kufikia mavuno ya juu zaidi na uwezekano bora wa kiuchumi kama mazao ya aina moj. Uwekezaji wa awali kwa ujumla ni wa juu zaidi kwa mifumo ya kilimo mseto. Hata hivyo, kuna manufaa kadhaaa ya mfumo wa kilimo mseto ambayo ni pamoja na; mazao ya kudumu hustahimili zaidi, na yanaweza kuzalisha kwa muda mrefu. Wakulima hunufaika na mazao ya pili kama chakula au kama chanzo cha mapato ambapo soko la bidhaa hizi linaweza kupatikana.
Faida za muda mrefu
Kilimo mseto hutoa mizizi zaidi ardhini, huboresha afya ya udongo na tija ya shamba kwa muda mrefu. Mizizi ya miti hulinda udongo dhidi ya mmomonyoko. Majani yaliyodondoka huongeza mboji ya udongo.
Miti kwa ujumla husaidia katika upenyezaji wa maji, pamoja na kuongeza uwezo wa udongo kushikilia maji. Miti pia hupunguza uvukizi na huboresha hali ya hewa shambani pamoja na kuondoa gesi mkaa (kaboni), jambo ambalo hupunguza mabadiliko ya hali ya hewa.
Mazingatio ya muda mrefu
Mimea ya yamii ya kunde hupunguza mahitaji ya mbolea kwani hutengeneza na kuongeza nitrojeni kwenye mazao. Ikilinganishwa na mimea ya aina moja iliyopandwa, mifumo wa kahawa na kakao una wachavushaji zaidi na viumbe-hai vyenye faida ambavyo hupunguza wadudu na magonjwa.
Utata wa kilimo mseto hakuhitaji tu vibarua zaidi vya awali bali pia ujuzi zaidi, ujuzi wa kitaalamu, ubunifu na ufanyaji wa maamuzi.
Usimamizi wa mandhari
Kwa manufaa kubwa zaidi za kilimo, tunahitaji kuangalia zaidi ya shamba moja tu. Mbinu bora za usimamizi wa mandhari wakati wa kushughulikia maswala muhimu ya mazingira, kijamii na hali ya hewa lazima zitekelezwe.
Unapaswa kujumuisha kilimo mseto na kuunganisha matumizi bora ya ardhi. Hili hutoa chaguo bora zaidi la kufikia malengo mengi ya upatikanaji wa chakula na mazingira bora.