Kuimarisha usimamizi wa mandhari

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=eUs4uruEUw4

Muda: 

00:05:15
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Agripreneurship Academy
Upandaji endelevu wa mazao pamoja na miti huongeza tija ya ardhi katika kipindi fulani, jambo ambalo huboresha kipato cha mkulima.
Ingawa mfumo wa kilimo mseto unavyosababisha mavuno mengi pamoja na uwezekano bora wa kiuchumi, uwekezaji wa awali kwa ujumla ni wa juu zaidi.

Utunzaji wa mandhari

Kwa kuwa na ustahimilivu pamoja na uwezo wa kuzalisha kwa muda mrefu, mazao ya kudumu huongeza mapato kwa mwaka mzima, na mizizi yake huboresha afya ya udongo. Mizizi ya miti hulinda ardhi dhidi ya mmomonyoko, majani yake huboresha mboji na pia miti huwezesha maji kupenyeza udongo pamoja na kuhifadhiwa vizuri udongoni.
Vile vile hupunguza uvukizi, na huboresha hali ya hewa katika mashamba.  Mimea ya jamii ya kunde hutengeneza na kutolea mimea mingine nitrojeni. Mfumo jumuishi wa kahawa na kakao una vichavushaji zaidi na viumbe-hai vyenye manufaa ambavyo hudhibiti wadudu na magonjwa. Ikiwa msongamano wa upandaji ni wa juu sana, unyevu unaotokea unaweza kusababisha magonjwa ya ukungu.
Zaidi ya hayo, ugumu wa utekelezaji wa kilimo mseto huhitaji ujuzi zaidi wa kitaalamu, kazi zaidi, ubunifu  na kufanya maamuzi sahihi. Ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kunahitaji juhudi za pamoja, kuimarisha kilimo hai na kupunguza ukataji ovyo miti.
Hatimaye, jumuisha kilimo mseto na unganisha matumizi sahihi ya ardhi na maeneo yenye thamani kubwa ya kiikolojia ili kufikia mfumo endelevu wa chakula unaostahimili zaidi.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:52Upandaji endelevu wa mazao pamoja na miti huongeza mavuno na mapato
00:5300:56uwekezaji wa awali kwa ujumla ni wa juu zaidi
00:5701:02Mfumo bora wa ikolojia unanufaisha mashamba ya kilimo mseto.
01:0301:25Mazao ya kudumu ni sugu zaidi na huzalisha kwa muda mrefu.
01:2601:56Kuna ongezeko na uwiano wa mapato kwa mwaka mzima.
01:5702:50Kupanda mseto husababisha mizizi zaidi ardhini na kuboresha afya ya udongo na tija kwa muda mrefu.
02:5103:05Mifumo jumuishi wa kahawa na kakao una vichavushaji zaidi na viumbe-hai vyenye manufaa
03:0603:17Ikiwa msongamano wa upandaji ni wa juu sana, unyevu unaotokea unaweza kusababisha magonjwa ya ukungu.
03:1803:27ugumu wa utekelezaji wa kilimo mseto huhitaji ujuzi zaidi wa kitaalamu
03:2803:40suala nyingine ni pamoja na uwepo wa kazi zaidi, ubunifu na kufanya maamuzi sahihi.
03:4104:39Ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kunahitaji juhudi za pamoja
04:4005:01Kujumuisha mbinu bora za matumizi ya ardhi ni muhimu ili kufikia mfumo endelevu wa chakula unaostahimili zaidi.
05:0205:15Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *