“ Kuhifadhi mboga za majani ya maharagwe“

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/conserving-bean-leaf-vegetables

Muda: 

00:11:00
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

NASFAM

Kula mboga ni muhimu kwa afya ya binadamu. Mboga zinaweza kuchunwa katika msimu wa mvua, na kukaushwa na kuhifadhiwa ili kutumika wakati wa kiangazi.

Majani ya maharagwe yana protini, vitamini A na C na madini muhimu kama ayoni na kalsiamu. Chuna majani laini yaliyokomaa vizuri kwa wakati wa wiki 7 baada ya kupanda. Acha kuchuna wakati maua yanapoanza kutokea.

Vyakufanya na vyakutahadhari

Hakikisha mimea imekomaa vizuri (kama wiki 7) kabla ya kuanza kuchuma. Chuna tu majani laini au nyororo, yenye afya wakati wa asubuhi. Acha muda wa wiki kadhaa baada ya kuchuna ili kuruhusu majani mapya kuchipuka. Acha majani kadhaa na uacha kuchuna kabla ya kutoa maua. Usichune majani yaliyokomaa sana au magonjwa. Usiyanyunyize majani ya kula madawa.

Kupika na kukausha majani.

Unaweza kukausha majani moja kwa moja, lakini watu wengi hupendelea kuyachemsha. Baada ya kuchuna, osha majani kwenye maji safi. Ondoa mashina na ukate majani katika vipande vidogo. Chemsha majani kwa muda wa dakika 20 na kisha uyatoe motoni. Toa majani kwenye sufuria ili yapoe. Yaweke kwenye kikapu kilicho na mashimo ili kudondosha maji.

Tandaza majani kwenye mkeka ulioinuliwa kutoka ardhini, kwenye jua. Geuza majani mara kwa mara ili yakauke kwa usawa. Baada ya kuyakauka vizuri, yahifadhi kwenye mipira ya majani, katika mahali pakavu.

Majani yanaweza kuliwa au kuuzwa wakati wowote wa mwaka. Majani ya malenge na majani ya kunde, pia yanaweza kuhifadhiwa kwa njia ile ile.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:23UtanguliziKula mboga kila siku ni muhimu kwa afya ya watu.
00:2401:06Majani ya maharagwe yana protini, vitamini A na C na madini muhimu kama ayoni na kalsiamu.
01:0701:15Katika msimu wa mvua, kuna majani mengi ya maharagwe. Unahitaji kuyahifadhi ili yapatikane wakati wa kiangazi
01:1601:26Majani yanaweza kuchunwa kutoka kwa maharagwe ya kutambaa na ya msitu.
01:2701:44Usinyunyize mimea na kemikali, na uhakikishe kuwa mimea imekomaa vizuri kabla ya kuanza kuchuna
01:4502:03Usichune majani 3 ya kwanza , na majani ya chini.
02:0402:50Chuna wakati wa asubuhi na uchune majani laini tu.
02:5102:56Acha ncha za majani zinazokua
02:5703:00Chuna tu majani yenye afya, yasiyo na wadudu.
03:0103:10Acha muda bila kuchuna kati ya mara mbili za kuvuna.
03:1103:39Acha majani kadhaa kwenye mmea, na uache kuchuna majani kabla ya mmea kutoa maua
03:4003:50Kiasi kinachosindikwa kinategemea ukubwa wa shamba, nafasi ya kukaushia, na uwepo wa jua.
03:5104:08Unaweza kuhifadhi majani kwa kuyakausha kwenye kikaushiaji cha jua. Watu wengine hupendelea kuchemsha majani kabla ya kuyahifadhi.
04:0904:23Tayarisha majani siku hiyo hiyo yaliyochunwa, lakini yakiachwa usiku kucha, yatandaze kwenye mkeka chumbani.
04:2404:32Mchakato: Andaa vyombo vya kupikia na mkeka safi, kavu.
04:3304:41Place the pot with little water on the fire.Weka sufuria iliyo na maji kidogo kwa moto.
04:4204:48Osha majani kwa maji safi.
04:4904:55Ondoa mashina na ukate majani katika vipande vidogo.
04:5605:02Weka majani ndani ya maji yanayochemka na ufunike
05:0305:09Yachemshe kwa dakika 20 kisha uyapinduwe mara moja.
05:1005:31Toa sufuria kwenye moto kabla ya majani kubadilisha rangi yake ya kijani
05:3205:40Toa majani kwenye sufuria ili yapoe
05:4105:45Yaweke kwenye kikapu kilicho na mashimo ili kudondosha maji
05:4606:14Baada ya kupoa, tandaza majani kwenye mkeka ulioinuliwa kutoka ardhini, ili yakauke.
06:1506:45Geuza majani mara kwa mara ili yakauke kwa usawa.
06:4608:07Yahifadhi kama mipira ya majani iliyokauka.
08:0809:18Weka mipira ya majani iliyokauka jikoni au kwenye sehemu nyingine kavu.
09:1909:38Majani ya malenge na majani ya kunde, pia yanaweza kuhifadhiwa kwa njia ile ile.
09:3911:00Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *