Kadiri mifereji inavyoharibika muda wa ziada, wakulima hupoteza rasilimali katika kazi za kila siku na kwa ajili ya ongezeko la uhaba wa maji na upungufu wa ubora wa maji, wakulima wanahitaji kuboresha matumizi ya maji.
Ili kuanzisha kikundi kipya, wanachama wanapaswa kujua kwamba kufanya kazi pamoja kunahitaji gharama, na hivyo wanapaswa kujadiliana pamoja ili kupata suluhisho na kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji. Teknolojia ni rahisi kufikia wakati wakulima wako kwenye kikundi.
Ushirikiano wa kikundi
Kwa ardhi iliyounganishwa, tengeneza alama za ardhi zinazoonekana ili kubainisha na kutambua kipande cha ardhi cha kila mmoja. Pia rasimisha ushirikiano kwa kuanzisha kampuni, au chama baadaye. Hata hivyo, anza kwa kukutana na wakulima wenzako na usikilize suala la kila mmoja wao, himiza mzunguko wa mazao na kikundi cha wakulima waliokaribu. Unda muundo wa kikundi ili kutenda kazi kwa ufanisi.
Vile vile, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya kazi kama kikundi, tafuta msaada kutoka kwa wakala wa ugani, na NGOs za kienyeji ili kuanzisha usimamizi na kujumuisha mikakati ya pamoja ya kilimo katika muundo sawa. Endelea kwa kukubaliana juu ya faida za michango ya hiari, na namna ya kufanya maamuzi na utatuzi wa mizozo miongoni mwa wanachama.
Zaidi ya hayo, kikundi lazima kiandike kanuni na sheria ya chama, na kutaja majukumu na wajibu wa wanachama na viongozi katika kikundi. Andika kazi ya kikundi na ripoti za kifedha.
Mwisho, wanachama wanapaswa kukubaliana juu ya bajeti na gharama za kazi za ziada, na mara nyingi wanachama wapange mikutano ili waweze kujenga uaminifu kati ya kila mmoja na kubadilishana mipango na kila mmoja.