Mbegu safi za ufuta zilizo na rangi sawa, ukubwa sawa, kiwango cha mafuta na wanga hupendekezwa. Hata hivyo, mazao ya ufuta hupungua ukichanganya aina tofauti.
Ufuta unapandwa kwa kupata mbegu za kula, na mapato kwa wakulima. Kufuata mbinu bora hupunguza kuchanganya aina tofauti za ufuta, na hivyo kuongeza ubora wake.
Mbegu bora
Badilisha mbegu ya ufuta kila baada ya miaka 3.
Tumia mbegu bora kutoka kwa wateja wanaoaminika, usichanganye mbegu wakati wa kuhifadhi na usitumie mbegu zilizomwagika kwenye sakafu kwa sababu zinaweza kuwa zimechanganywa aina.
Hifadhi aina tofauti kwenye maghala tofauti na shughulikia ugawaji na usambazaji wa mbegu tofauti kwa wakulima.
Usipande zaidi ya aina moja ya ufuta shambani. Safisha shamba kabla ya mimea kuchana maua kwa kuondoa aina zingine za ufuta pamoja na mimea iliyoathiriwa na ugonjwa.
Acha umbali mrefu kati ya mashamba 2 yaliyokuza aina tofauti za ufuta ili kuzuia wadudu kusambaza chavua kutoka shamba moja hadi jingine.
Vuna aina tofauti kivyake, na safisha vyombo vya kuvunia kabla ya kutoka shamba moja kwenda jingine lililo na aina tofauti.
Andaa sehemu tofauti ya kukaushia na kupuria pamoja na kusafisha zana za kupuria.
Weka punje katika gunia bora. Funga gunia na weka alama ya jina ili kubainisha aina iliyomo. Weka kila aina katika ghala tofauti. Hakikisha kwamba magunia ya ufuta hayashambuliwi na panya ambao wanaweza kuchanganya mbegu.