Virusi vya kukunja majani ni ugonjwa haribifu ambao husababisha hasara kubwa kwaani, ni muhimu kuudhibiti. Ikiwa umedhibitiwa vizuri, mboga huleta mapato zaidi.
Virusi vya kukunja majani husababishwa na virusi, husambazwa na nzi weupe amabao hufyonza utomvi kutoka mmea mmoja hadi mwengine. Ugonjwa huo hushambulia nyanya, koliflawa, biringani, viazi na tumbaku. Majani mapya ya mmea ulioathirika huwa madogo, yamekunjika, na hujikuja kupinda juu. Maua hudondoka kabla ya kuzaa matuda, na mimea iliyoathirika hudumaa.
Kudhibiti nzi weupe
Kudhibiti nzi weupe ni hatua muhimu ya kupigana na ugonjwa huo. Ni vigumu kudhibiti nzi weupe kwa kutumia viuawadudu.
Linda miche dhidi ya nzi weupe kwa kufunika kitalu katika wavu au chandarua. Panda mimea mitego kama mahindi, mtama, wimbi na mawele. Mimea yenye harufu kama vile giligilani, dania, hawaji, shamari na mnanaa ambayo huwafukuza nzi weupe, kwaani panda mimea hii kando ya shamba lako. Tunza wadudu wazuri kama dudu kobe na nyigu ambao huwaua nzi weupe, kwaani panda mbangimwitu kuwavutia.
Tumia mitego ya kadi za manjano ambayo huwavutia nzi wazuri. Ikiwa hazipatikani kwa urahisi, jitengenezee mitego mwenyewe. Nyunyizia dawa ya asili asubuhi au jioni ukitumia tangawizi, kitunguu saumu na pilipili. Katika hatua ya mwanzo ya ukuaji, nyunyiza kwa kutumia mafuta ya mwarobaini ili kuzuia shambulio la nzi weupe.
Usimamizi wa ugonjwa
Panda aina sugu. Tumia mbegu kutoka kwa mimea yenye afya.
Ongeza samadi au mboji. Ng‘oa na kuchoma mimea iliyoathiriwa.