Ulimwenguni kwote, mihogo hukuzwa kwa wanga na mizizi yake inayoliwa, lakini huathiriwa na wadudu na magonjwa. Matekenya ni moja wapo ya wadudu wakubwa ambao hushambulia mihogo, na wanahitaji kudhibitiwa.
Kuna aina nyingi ya matekenya, wote wakiwa na maumbo tofauti. Wanaweza kuwa weupe, wekundu au kijani. Wote wanaweza kudhibitiwa kwa njia sawa. Matekenya wanaweza kuenezwa kupitia upepo, maji na wanadamu. Mimea ya mihogo iliyoshambuliwa hutoa mizizi midogo.
Kudhibiti matekenya
Matekenya wanaweza kudhibitiwa na kuzuiwa kwa mbinu kadhaa ambazo ni pamoja na kuondoa na kuchoma mabaki ya mimea iliyoathiriwa baada ya kuvuna. Hii huzuia upitishaji wa matekenya kwa msimu ujao. Kupanda mazao mengine kama vile mahindi, miwa au mazao yoyote yasiyopokea matekenya. Unaweza tena kupanda mihogo baada ya mazao mengine kuvunwa. Panda mapema katika mwanzo wa mvua, kwani maji hudondosha matekenya. Kwa hivyo, kunasalia matekenya wachache kwa mimea, au wote huondolewa.
Awali, panda mbegu zenye afya na zilizowekwa kwenye dawa ili kuua viini. Hatua hizi hufanywa ili kuwezesha kupanda mbegu ambazo hazina matekenya. Kukagua shamba mara kwa mara katika msimu wote ili kuondoa ncha zilizoathiriwa na matekenya hupunguza magonjwa kuenea. Mabaki ya mimea na vipande vilivyoondolewa huchomwa ili kuua matekenya.