Chule ni ugonjwa hatari wa kuvu ambao huathiri maembe. Chule hustawi vizuri katika hali ya mvua na unyevu. Ugonjwa huu unaweza kudhibitiwa kwa kupogoa, na kutumia viuakuvu.
Ugonjwa huu husababisha uharibifu mkubwa shambani, lakini pia huharibu matunda baada ya kuvuna, na hivyo ni changamoto kubwa kwa soko la kuuza nje.
Chule hutambuliwa na uwepo wa madoa meusi kwenye majani ambao huwa madogo awali, na baadaye hupanuka. Chule husababisha mashimo kwenye majani, ambayo hukauka mwishowe. Ugonjwa huo huenezwa kupitia kwa mvua, na maambukizo huanzia kwa majani, huenea kwa matawi, na kisha kwa maua na mwishowe mmea wote.
Hatua za udhibiti
Kagua shamba lako mara kwa mara na ufuatilie mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu chule hudhuru sana baada ya mvua.
Ondoa sehemu zilizoambukizwa, haswa maembe madogo na yaliyooza. Hizi hufanya kama chanzo cha kueneza ugonjwa.
Pogoa matawi ya mti ili kuwezesha upenyezaji wa mwanga wa jua. Hii huzuia hali ya unyevu ambayo husababisha chule.
Matumizi ya dawa ya viuakuvu
Kuyunyiza viuakuvu tu haitoshi, bali ni bora kuvitumia pamoja na udhibiti wa mikono. Viuakuvu vinaweza kuwa vya mugusano (viuakuvu vya shaba) au vya kimfumo. Tumia viuakuvu vya shaba wakati dalili za ugonjwa za kwanza zinapoonekana, na viuakuvu vya kimfumo muda mfupi kabla ya maua kutoka. Walakin, usitumie viuakuvu wakati wa maua kuchana, kwasababu huwa vitaharibu maua. Endelea kunyunyizia dawa kila baada ya wiki 3 hadi 4, huku ukibadilisha kati ya viuakuvu vya kimfumo na vya msugano.
Sitisha kunyunyizia viuakuvu hivyo wiki 3 kabla ya kuvuna, lakini waweza kutumia vile vilivyo na viambato tofauti.
Changanya rangi ya chakula na maji, na umwagiliae mchanganyiko huo kwenye mti kutoka juu hadi chini. Tahadhari kuangalia ni kiasi gani kinachotumika. Panua kiwango hiki ukitegemea idadi ya miti uliyonayo ili kukadiria kiwango cha kemikali kinachohitajika.