Ikiwa unajua kutambua na kutoa viwavijeshi, basi ni rahisi kuwadhibiti.
Viwavijeshi, mara nyingi hujeficha ndani kabisa ya shina la mahindi ambapo dawa haziwezi kuwafikia na kuwaua. Kwa hivyo, lazima wakulima wawatafute na kuwaua ili waweze kupata mavuno. Viwavijeshi hupenda kula majani ya mahindi, lakini pia wanaweza kuishi katika mimea mingine. Wanaanza na kula madirisha madogo kwenye majani, amabao huendelea kugeuka matundu makubwa.
Maisha ya nondo
Nondo wa viwavijeshi anaweza kupaa umbali mrefu , na pia hutaga hadi mayai 200 kwenye jani moja. Unaweza kutambua mkusanyiko wa mayai ya nondo ambao kwamba waweza kuwa na ukubwa uliolingana na kidole kigumba na hufunikwa na manyoya laini meupe.
Siku 3 baada ya kutaga, viwavijeshi wadogo huanguliwa kutoka kwenye mayai, wanakwaruza majani wakitambaa na hivyo huacha madirisha madogo kwa majani. Na kwa siku 3 zijazo, huwa wanatafuata shina la majani kujificha. Katika wakati huu, madirisa hugeuka matundu makubwa kwasababu viwavijesha huwa wamekua wanono. Ukifunua shina la majani , unaweza kumpata kiwavijeshi kimoja tu, kwasababu huwa wanawala wenzao ili kupunguza kushindania chakula.
Baada ya wakati wawiki 2-3 , viwavijeshi huondoka huanguka kwa ardhi. Kisha wakichimba umbali usiozidi urefu wa kidole ardhini, ambapo hujifunika kwa kifukofuko cha rangi ya hudhurungi.
Wiki mbili baada ya hapo, nondo mzima hutoka kwenye hiki kifukofuko, hupaa na huanza kutaga mayai mapya,
kuua viwavijeshi kwa mkono
Tembelea shambani lako kila asubuhi baada ya siku 3 katika wiki 6 za kwanza, na ukague kama kuna ishaara zozote za shambulio la wadudu. Unapoona kinyesi cha mayai, basi kunjia mayai haya kwenya majani na kuwavunja na mkono wako.
Unaweza pia kueka kijiko kimoja cha udongo, jivu au mchanga kwenye china la mmea ili kuua viwavijeshi.