Malisho ni moja wapo ya sababu kuu zinazoathiri ufugaji wa mifugo, na huamua ubora na wingi wa bidhaa za mifugo zinazozalishwa.
Mifugo hutoa mayai, nyama, maziwa na kipato kwa wafugaji, kwa hivyo malisho duni huathiri uzalishaji wa bidhaa za mifugo, kwani husababisha upungufu kwa uzito wa mifugo, upungufu wa uzalishaji wa maziwa, uzalishaji wa maziwa yenye mafuta kidogo, upotezaji wa rangi ya manyoya na magonjwa ya ngozi. Chakula kilichosawazishwa kama vile malisho ya kijani kibichi, chakula cha madukani, chumvi na madini hutoa virutubisho vinavyohitajika kwa mifugo.
Uzalishaji wa malisho
Machipukizi ni nafaka zilizolowekwa kwenye maji na kuachwa ziote. Machipukizi ni rahisi kumengenywa kuliko nafaka na yanaweza kuzalishwa kwa mwaka mzima. Hayahitaji ardhi wala chumba kuzalishwa na yanaweza kupatikana kutoka kwa nafaka yoyote.
Loweka vipande 3 vya kitambaa kwenye maji, kamua vitambaa ili kuondoa maji ya ziada, vitandaze ardhini na kisha tandaza nafaka 50 juu ya kitambaa kwa muachano wa kidole 1. Kisha kunja upande mwingine wa kitambaa ili kufunika nafaka. Loweka tena kitambaa mara kwa mara ili kiwe na unyevu na baada ya siku 2-3 fungua kitambaa ili kuangalia kama nafaka zimeota, na kisha hesabu asilimia ya uotaji.
Ili kuzalisha machipukizi, tumia nafaka bora na uziweke kwenye chombo, ongeza chumvi kidogo, maji safi na uondoe mbegu zinazoelea. Nafaka hulowekwa kwa masaa 12, na kuwekwa kwenye kivuli na kisha maji huondolewa. Weka nafaka kwenye mfuko safi wa pamba, kisha uufunge ili kutoa joto ndani na uhifadhi mfuko chumbani au kivulini. Katika hali ya hewa ya joto, nafaka huchukua masaa 26-18 kuota.
Fungia begi kwenye blanketi na mara nafaka zinapoota, ziondoe kwani ziko tayari kulisha wanyama. Lisha 1/2 kg ya machipukizi kwa kila ng’ombe mara moja kwa siku pamoja na malisho mengine.
Hatimaye, mpe kondoo mkono 1 au 2 uliojaa machipukizi mara mbili kwa wiki, na ulishe kuku 10 mkono 1 wa machipukizi uliojaa mara moja kwa siku.