Kuna mambo na mazingatio ambayo yanahitajika wakati wa kuchagua eneo la kufugia nyuki kwa uzalishaji bora wa kiuchumi, afya ya nyuki na usimamizi wa rahisi.
Jambo kuu linalozingatiwa wakati wa kuchagua eneo la kufugia nyuki ni upatikanaji wa chavua na mbochi bora. Hii ni kwa sababu nyuki wa asali wanahitaji mlo kamili wa mbochi, chavua na maji. Chagua maeneo yenye aina kuu za mimea ambazo zinachanua maua.
Mambo mengine
Eneo linapaswa kuchaguliwa karibu nyumba ili kurahisisha usimamizi. Ufikiiaji wa eneo ni muhimu sana kwa hiyo, epuka maeneo ya mbali ambayo ni vigumu kuyafikia au yale ambayo yanaweza kuathiriwa na mafuriko.
Eneo linaweza kupatikana kutoka kwa mali ya kibinafsi kwa kuomba idhini kutoka kwa mmiliki. Ni hatua nzuri ya kibiashara kwa mmiliki wa biashara kuchukua bima ya dhima ya umma na bima ya moto wakati mizinga yapo kwenye ardhi ya kibinafsi na ya serikali.
Eneo zilizo wazi zinapendekezwa, lakini eneo zinazotoa kivuli ni bora katika hali ya hewa ya joto. Ni muhimu kuzuia na kudhibiti wadudu waharibifu kama vile mchwa na chura.
Maeneo ya kuepuka
Epuka maeneo ambayo hufurika maji, na maeneo yaliyo na uwezo mkubwa wa kushambuliwa na moto.
Epuka kuweka mizinga ya nyuki karibu na milango, zizi la mifugo, maeneo ya kunyweshea wanyama, mabwawa, na kambi.
Epuka kuweka mizinga ya nyuki katika maeneo ambayo yanafikiwa na viua wadudu. Ni muhimu pia kutoweka mizinga ya nyuki karibu na viwanda vya kusaga chakula, viwanda vya sukari, viwanda na malisho kwani nyakati fulani nyuki huzurura kwenye maeneo kama hayo kutafuta chavua au sukari. Pia epuka kuweka mizinga ya nyuki karibu na msongamano wa watu.