Jiko la mkaa hutumika kukaushia samaki. Sehemu zalo ni pamoja na chumba cha mkaa, na trei ya moshi ambapo samaki huwekwa ili kukauka.
Ujenzi wa jiko la mkaa
Jiko la mkaa linaweza kujengwa kwa matofali ya udongo, matofali ya saruji, na matofali yaliyochomwa.
Ili kutengeneza jiko la mkaa kwa kutumia matofali ya zege, utahitaji brashi, nyundo, kamba, jembe, mwiko, rula ya mraba.
Kabla ya ujenzi, unahitaji kwanza kuamua ukubwa wa jiko na aina ya vifaa unahitaji kutumia.
Jiko la mkaa kawaida huwa na ukubwa mraba wa mita 1 na unene wa ukuta kawaida ni sentimita 16.
Jiko la mkaa linaweza kuwa na sehemu 1 au zaidi kila sehemu ikiwa na ukubwa wa mita 1 ya mraba.
Iwapo unatengeneza jiko kwa kutumia matofali yenye mashimo, hakikisha kumwaga udongo au mchanga kwenye mashimo ili jiko liweze kuhifadhi joto.
Lango la eneo la moto linapaswa kuwa 35cm kwa urefu na upana.
Baada ya kutengeneza umbo la jiko la mkaa, wavu wa nyaya huwekwa juu ambapo samaki watawekwa.