Aina ya kakao huamua msimu wa uzalishaji, ubora na wingi wa mavuno, udumifu na upinzani dhidi ya wadudu na magonjwa.
Kubebesha miche ya mikakao huboresha uzalishaji wake, na hufanywa kwa kutumia njia 3 ambazo ni; ubebeshaji wa pembeni ya shina, ubebeshaji kwa fundo moja, na ubebesha wa mpasuko.
Vifaa vya kuunganisha miche ni pamoja na kinyunyizio, kisu cha kupandikiza, mkasi, karatasi ya plastiki, vifungashio.
Mbinu za kuunganisha
Kabla ya kuunganisha, safisha vifaa, chagua mche shina ulio na afya na nguvu. Pata kikonyo kutoka kwa tawi lililo majani na vijicho vilivyokomaa.
Kata tawi yaliyo na vifundo 3–6 kutoka kwa ncha, ondoa majani, iweka kwenye mfuko wa plastiki na uichukuwe haraka kwa mahali utakapobebeshea ili kupunguza upotevu wa maji.
Kwa ubebeshaji wa pembeni ya shina; tayarisha mche shina na ufanye mkato kando. Kisha, kata sehemu ya juu ya mche shina. Baada ya hayo, tayarisha kikonyo, fanya mkato uliyochonga na kisha ingiza kikongo ndani ya mkato ulio kwenye mche shina na ufunge sehemu iliyokatwa ukitumia karatasi ya plastiki.
Kwa ubebeshaji wa fundo moja; Kusanya kikonyo na uondoe majani. Tayarisha mche shina na ufanye mkato mfupi kutegemea urefu wa kikonyo. Fanya mkato uliyochonga kwa upande mmoja wa kikonyo na mkato pima urefu wa kikonyo, kwa upande mwengine. Kisha kata kikonyo juu ya mkato uliyochongoka. Chomeka kikonyo(kijicho) katika mche shina na uifunge.
Ubebeshaji wa mpasuko hufaulu katika kiangazi wakati halijoto ni ya juu na mvua ni kidogo.
Kwa ubebeshaji wa mpasuko, kusanya kikonyo, ondoa majani, fanya mkato uliyochonga kulingana na inchi 1.5. Tayarisha mche shina kwa kukata sehemu ya juu ya mmea kwa urefu wa inchi 68 kutoka kwa msingi wa mmea.
Endelea kwa kufanya mkato wa kina cha inchi 1.5 juu ya mche shina na uingize kikonyo. Funga kwa kutumia karatasi ya plastiki na vifungashio, ambavyo huondolewa baada ya miezi 2 wakati kubebesha kumefanikiwa.
Hatimaye, Ondoa mmea shina mara tu majani ya kikonyo kilichobebeshwa yanapokomaa. Pia uondoe machipukizi yoyote mapya yanayochipuka kutoka kwenye mmea.