Ufugaji wa kuku ni biashara nzuri ambayo huhitaji mtaji mdogo na hutoa faida kubwa kwa muda mfupi.
Baada ya kuanzisha ufugaji wa kuku unashauriwa sana kuchukua hatua nzuri za usalama ili kuzuia uenezaji wa magonjwa pamoja na vifo vya ndege. Pia utunzaji mzuri wa kumbukumbu unashauriwa kwa wafugaji wa kuku, kwani husaidia kuwafahamisha iwapo shamba linapata hasara au faida. Kuna vifaa na mashine kadhaa vinavyohitajika kwa ufugaji wa kuku, na hivyo ni pamoja na vihori vya kulishia na kunyweshea, vifaa vya kutotolesha mayai, na mtambo wa kusaga chakula.
Kanuni za kimsingi
Anza kwa kufanya utafiti kuhusu vipengele mbalimbali muhimu vya ufugaji kuku kama vile mbinu za ufugaji, aina ya kuku, na vyanzo vya vyakula.
Baada ya hapo, tengeneza mpango wa biashara ili kusaidia katika kufikia malengo ya biashara, na hivyo kuwa na mwongozo wa biashara.
Pia pata mtaji wa kukidhi gharama mbalimbali kama vile kununua ardhi, kujenga banda, kununua vifaa, kununua chakula na kulipa wafanyakazi.
Pata kipande kikubwa cha ardhi katika eneo lisilo la karibu na makazi ya watu, lisilotwamisha maji, na kisha ujenge banda.
Pata vifaa, mashine na sajili biashara ya ufugaji wa kuku katika.
Ajiri wafanyakazi na uwafunze, kisha pata vifaranga na uanze kujiandaa kuvitunza.
Hakikisha umeweka dawa ya kuua viini katika kila banda, fuata mbinu bora za usimamizi na shauriana na wataalam ili kuepuka hasara kwa kuwa hatua ya kutunza vifaranga ni hatua muhimu sana.
Anza kutafuta soko mara tu vifaranga wanapofika shambani ili kuuza kuk.u kwa wakati ufaao.