Kutayarisha dawa ya kuua wadudu
Kwanza, weka kijiko 1 cha poda ya manjano kwani ina kipengele ambacho huzuia magonjwa ya ukungu na ya bakteria. Ongeza kijiko cha sinamoni, pilipili nyekundu na kijiko 1 cha mafuta. Chemsha mchanganyiko kwa muda wa saa moja na uiondoe. Acha mchanganyiko upoe kisha uchuje. Ongeza maji kwenye mchangayiko kwa uwiano wa 1: 3.
Mwishowe, weka mchanganyiko kwenye chupa na kunyunyizia mimea.