Kingamaji ni muhimu kwa kulinda shamba dhidi ya mmomonyoko. Kingamaji husaidia wakulima kupata mavuno mengi na pesa zaidi.
Kwenye ardhi ya mteremko, kuna mtiririko wa maji mengi ambayo husababisha mmomonyoko wa udongo wa juu wenye rutuba. Maji yanayotiririka hubeba chembe nyororo ya udongo ambayo huziba safu ya ardhi. Wakati udongo umeganda, maji ya mvua inayofuata hupita kasi juu ya ardhi, na hivyo maji kidogo tu hupenyeza kwenye mchanga.
Kingamaji
Kingamaji ni matuta ya kudumu yaliyotengenezwa kutoka ardhini. Wanajengwa na mwinuko kuhakikisha kwamba maji hutiririka polepole. Kwa hivyo, maji yanaweza kupenyeza udongo. Unaweza kuanza kupanda mazao baada ya mvua ya kwanza, kisha mbegu huchipuka vizuri na miche huathiriwa kidogo na kiangazi.
Jinsi ya kufunga kingamaji
Anzia juu ya shamba. Tengeneza kingamaji la kwanza umbali wa mita 25 chini ya upande wa juu ya shamba. Kwenye mteremko mpole, tengeneza kingamaji ukiacha umbali wa mita 50 baina yao. Kwenye mteremko mkali unahitaji kufanya kingamaji zikaribiane.
Shikilia mguu mmoja wa A-frame kwa msimamo. Kisha, punga mguu mwingine kuzunguka A-frame hadi A-frame iwe na kiwango kizuri. Pigilia kigingi ardhini. Baada ya hapo, punga mguu mwingine wa A-frame. Rudia mchakato hadi uwe umepiga mstari wa kwanza wa kingamaji katika shamba. Lainisha pembe kali ili kufanya kilimo iwe rahisi.
Kwenye udongo wa kunata, lima mara mbili pande zote za mstari wa kingamaji. Ili kutengeneza kingamaji, tupa udongo uliolimwa kwa mistari ya nje juu ya mistari ya ndani. Kwenye kingamaji za mchanga, lima angalau mara tatu kando ya mistari ya kingamaji. Lazima bana kingamaji za mchanga, ili ziwe imara.
Wacha mifereji kwa pande zote mbili za shamba zifunguke, ili maji yanapozidi yatoke nje. Unaweza kuimarisha kingamaji kwa mawe au nyasi.