Upandaji miti ni mchakato wa kupanda misitu mipya kabisa ambapo hapakuwa na miti wowote.
Msitu uliopandwa unaweza kuunda makazi mapya ya wanyamapori, kuunda kazi na faida za kiuchumi kwa jamii, na pia kuongeza uwezo wa sayari wa kuondoa kaboni dioksidi (hewa ukaa). Upandaji miti una aina tatu yaani urejeshaji asilia, kilimo cha miti kibiashara na kilimo mseto cha miti na mazao.
Aina za kilimo miti
Urejeshaji asili. Hapa ndipo misitu hupandwa na kuachwa peke yake kwa muda mrefu sana. Hii ndiyo misitu yenye ufanisi zaidi katika kuondoa kaboni na kuunda makazi mapya ya wanyama. Hii hutokana na uwepo wa aina mbalimbali za miti ambavyo husababisha dari kubwa, na uwezo mkubwa wa kunasa mwanga wa jua.
kilimo cha miti kibiashara. Hapa ndipo misitu inapandwa lakini kwa bidhaa maalum kama mbao au kwa ajili ya kutengeneza karatasi. Msitu huo pia una ufanisi mzuri katika kuondoa kaboni, ingawa miti hatimaye huvunwa.
Kilimo mseto. Hiki kinahusisha upandaji wa miti pamoja na mazao, na ufugaji wa wanyama. Hiki ni chanzo muhimu cha chakula na mapato kwa jamii, lakini wakati mwingine husababisha ukataji miti ovyo wakati miti inapokatwa ili kutengeneza ardhi kwa ajili ya kupanda mazao.
Hatari na changamoto
Upandaji miti kwa kiwango kikubwa unaweza kusababisha mabadiliko ya matumizi ya ardhi ambayo husababisha ushindani wa ardhi na hivyo kuongezeka kwa bei ya chakula.
Kuchagua aina sahihi ya upandaji miti ni muhimu ili kuhakikisha kuwa jamii zinanufaika.
Miti inahitaji kutunzwa baada ya kupandwa ili kuhakikisha uhai wake, na hii pia ni pamoja na kulinda miti dhidi ya ukataji ovyo.