Kilimo hai cha choroko (moong)

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=HsATiBYgb5A

Muda: 

00:10:44
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Agri Farming
Mmea wa moong dal unaojulikana kama choroko ni zao muhimu la familia ya fabaceae. India ni mojawapo ya waagizaji wakubwa, wazalishaji na watumiaji wa mikunde.
Mikunde nchini India hulimwa kwa kutumizi gharama nafuu na rasilimali kidogo ikilinganishwa na ufugaji wa wanyama. Miongoni mwa mikunde, choroko ni chanzo cha protini ya ubora wa juu, na hutumiwa kama nafaka. SSL 1827 ni aina ya choroko iliyotengenezwa kwa kuunganisha maharagwe, mchele na choroko. Aina hiyo ni sugu dhidi ya magonjwa ya virusi. Aina nyingine ni ML 2056, SML 666, SML 832 na DMB 37.

Masharti

Choroko hustawi vizuri katika mwinuko wa 0-1600m juu ya usawa wa bahari na chini ya hali ya hewa ya joto nyuzi 20-30.
Choroko hustawi katika udongo wa mwekundu wa tifutifu, lakini pia hustawi vyema kwenye udongo usio na kichanga kingi. Choroko hazistawi katika udongo wenye unyevu wingi sana. Choroko zinaweza kulimwa katika aina mbalimbali za udongo, na mavuno bora hupatwa kutoka kwenye udongo tifutifu usio na maji mengi.

Usimamizi wa udongo

Kiwango cha ph bora zaidi kinapaswa kuwa 6.5 hadi 7.5. Maandalizi ya ardhi kwa ajili ya upandaji wa choroko yanahitaji kilimo-hai, kwani hakuna haja ya kutengeneza kitalu cha mbegu.
Choroko hupandwa kwenye udongo wenye kina kirefu. Unapolima hakikisha kwamba unachanganya vizuri mbolea na samadi kwenye udongo. Huku huzuia ukuaji wa magugu na husaidia mbegu kuota vizuri, pamoja na kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuhifadhi unyevu wa udongo.

Udhibiti wa wadudu

Wadudu maarufu zaidi wanaopatikana katika choroko ni nzi wa shina, ambao huathiri mmea katika hatua za awali na hivyo kusababisha kukauka na kunyauka kwa mimea.
Nzi hudhibitiwa kwa kunyunyizia mafuta ya mwarobaini na dawa za kuua wadudu. Unaweza pia kuwadhibiti kwa njia ya kikaboni kwa kuwaondo kwa kutumia mikono au kutumia mbinu jumuishi ya kudhibiti wadudu. Vuna choroko wakati asilimia 85 ya ganda la mbegu limekomaa, na hii hufanywa kwa kuchuma kwa mara 2-5 kwa wiki.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:00Mmea wa moong dal unaojulikana kama choroko ni zao muhimu la familia ya fabaceae.
01:0102:06Udongo bora kwa kilimo cha choroko
02:0703:00udongo usiofaa kwa kilimo cha choroko
03:0104:00Unapoima, changanya mbolea na samadi kwenye udongo.
04:0105:00Muachano unaofaa taki ya mimea
05:0106:00Maandalizi ya ardhi
06:0106:55Matumizi ya samadi au mbolea husababisha mavuno bora
06:5607:50Mfumo jumuishi wa matumizi ya virutubisho husaidia kudumisha na kuboresha rutuba ya udongo
07:5108:40Matumizi sahihi ya mbolea huboresha mavuno
08:4109:30Wadudu maarufu zaidi wanaopatikana katika choroko ni nzi wa shina
09:3110:10Vuna choroko wakati asilimia 85 ya ganda la mbegu limekomaa
10:1110:44Uvunaji kabla ya kukomaa husababisha ubora duni, mavuno kidogo. Mbegu ambazo hazijakomaa zina wezekano mkubwa wa kushambuliwa wakati wa kuhifadhi.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *