Tangawizi ni mmea wa familia ya zingibaraceae. Ukuaji wa tangawizi kwa njia ya hidroponiki hutoa faida zaidi kuliko njia nyingine za kilimo.
Hatua ya kwanza ni kupanda tangawizi kutoka kwa kipande cha mzizi kilicho na kijicho au chipukizi. Ni muhimu kupanda awali kwenye udongo wenye mboji, na kisha uhamishe miche kwenye mfumo wa hidroponiki baadaye. Katika mfumo wa hidroponiki, maji hurejeleswa tena. Maji yanayotiririka hutegwa na kurudishwa kwenye mfumo. Upotevu wa maji hutokea kwa namna mbili ambazo ni; kupitia uvukizi na uvujaji wa mfumo.
Faida za hidroponiki
Mimea iliyopandwa kwa njia ya hidroponiki hukua haraka hadi 50% kuliko mimea iliyopandwa kwenye udongo. Hii ni kwa sababu ya virutubisho vya mara kwa mara vinavyopatikana katika mfumo wa hidroponiki. Mazao mapya yanaweza kupandwa mwaka mzima. Mfumo wa hidroponiki huondoa hitaji la viuatilifu na viuawadudu. Mimea kwenye mfumo huo hutumia 10% tu ya maji ikilinganishwa na mimea ya shambani.
Kwa kuongeza, mimea hupandwa karibu na hivyo nafasi ndogo hutumiwa. Wakulima pia wanaweza kuzalisha chakula kwa wakati unaofaa ili kuongeza faida. Na pia mtu ana udhibiti kamili wa joto, unyevu, mwanga na hewa.