»Kilimo cha Soya«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=DDwjeckDLGM

Muda: 

00:09:52
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Ghana E-Agriculture

Soya ni zao muhimu la jamii ya kunde ambalo huweka nitrojeni kwenye udongo, hufanya kama mbadala wa nyama, hufanya kama kiungo cha kutengeneza tom brown, na hutoa mafuta.

Kupanda mimea ya soya kwa ukaribu husaidia kupata idadi nzuri ya mimea, urefu wa juu wa mmea, na mavuno mazuri. Hata hivyo, epuka kupanda mimea mapema au kuchelewa sana kati msimu kwani hii husababisha mavuno duni. Kwa soya iliyotayari kuvunwa, maganda na majani yake hubadilika rangi ya manjano, mbegu huwa ngumu na manjano.

Kilimo cha soya

Chagua udongo tifutifu uiliopata mvua isiyo chini ya 700mm.

Fyeka manyasi, na ulime udongo ili kuvunjavunja mabonge ya udongo. 
Acha mimea iliyokatwa shambani ili kufanya kama matandazo, ambayo kudhibiti mmomonyoko wa udongo, kudumisha halijoto nzuri ya udongo na kuboresha viumbe hai. 
Chagua mbegu zilizoidhinishwa zinazotoa mazao mengi, zinazostahimili magonjwa, zinazostahimili mipasuko ya maganda, zinazokomaa mapema na zinazostahimili ukame kutoka kwa wafanyabiashara wanaoaminika. 
Pima uotaji na nguvu ya mbegu ili kusaidia kujua ubora na kiwango cha mbegu kinachohitajika kupandwa. Iwapo 85% itaota panda mbegu 2, kwa 70 – 84% panda mbegu 3, lakini ikiwa chini ya 70% usipande mbegu hizo. 
Changanya mbegu na chanjo ili kuzuia bakteria kufa, na panda kwa kina cha 3cm, umbali wa 75 cm kati ya safu na 5cm kati ya mimea. 
Weka mbolea ya fosforasi, mbolea ya potasiamu na mbolea ya kikaboni kama ziada. 
Ondoa magugu wiki 2–3 na wiki 5–6 baada ya kupanda ili kupunguza ushindani wa virutubisho. 
Dhibiti wadudu na magonjwa kwa kutumia aina sugu za mbegu zinazostahimili, na fanya mzunguko wa mazao. 
Vuna kwa wakati sahihi, kausha, pura, safisha na kausha tena ili kuhakikisha ubora wa nafaka.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:29Soya huweka nitrojeni kwenye udongo, hufanya kama mbadala wa nyama, hufanya kama kiungo cha kutengeneza tom brown, na hutoa mafuta.
01:3001:33Kilimo cha soya
01:3402:08Chagua udongo tifutifu uiliopata mvua isiyo chini ya 700mm.
02:0903:22Fyeka manyasi, lima udongo na acha mimea iliyokatwa shambani
03:2304:12Chagua mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wafanyabiashara wanaoaminika.
04:1305:21Pima uotaji na nguvu ya mbegu siku 10 kabla ya kupanda.
05:2207:02Changanya mbegu na chanjo, panda mimea karibu.
07:0307:55Weka mbolea ya fosforasi, mbolea ya potasiamu na mbolea samadi.
07:5608:16Ondoa magugu wiki 2–3 na wiki 5–6 baada ya kupanda
08:1709:12Dhibiti wadudu na magonjwa
09:1309:52Vuna kwa wakati sahihi, kausha, pura, safisha

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *