Mmea wa nyanya unapaswa kuwa na mizizi iliyokua vizuri ili uweza kuhimili majani na matunda. Mizizi dhaifu husababisha uozo kutokana na mkusanyiko wa maji karibu na mizizi.
Unapopandikiza, usichimbe mashimo ya kina kirefu ili mizizi isiingie sana kwenye udongo. Dumisha hali nzuri katika kitalu ambayo inaweza huwezesha mimea kustawi vyema. Katika banda kitalu, mkulima anapaswa kuwa na mfumo mzuri wa umwagiliaji wa maji. Mwagilia mimea maji kwa muda mfupi kila saa kwa siku ili kuepuka kumwagilia kupita kiasi.
Kusawazisha kati ya udongo na maji
Bonyeza udongo kwenye kiganja ili kuangalia kiwango cha unyevu. Joto linapokuwa juu, nyunyizia mimea maji zaidi ili kuhakikisha udongo unapata unyevu wa kutosha. Ili kuhakikisha matokeo bora, sawazisha kati ya maua na matunda, shina na majani.
Kupogoa ni muhimu; kwa kuondoa na majani mazee, tunda la nyanya litakua baada ya kila majani matatu. Kupogoa kunapaswa kufanywa wakati nyanya ziko tayari kuvunwa. Pogoa majani yanayogusana na ardhi. Vuna nyanya ukiacha kijiti ambacho hushikilia tunda ili kuongeza maisha ya kuhifadhi tunda.
Udhibiti wa wadudu
Nyanya hukabiliwa na magonjwa na wadudu. Ili kuzuia magonjwa tumia mbinu asili, kagua mimea, dumisha usafi shambani na tumia kemikali. Magonjwa haya mara nyingi huhusishwa na mgusano wa mmea na udongo.
Wadudu ni pamoja na nzi weupe na chawa. Ili kudhibiti wadudu, tumia mitego ili . Mitego ya manjano hunasa inzi weupe, huku mitege ya bluu hunasa chawa. Wadudu wengine hudhibitiwa kwa kutumia kemikali maaalum. Ukitengeneza mazingira mazuri kwa mazao yako yatafanya vizuri hadi kukomaa.