Wakulima wengi wamekumbatia matumizi ya banda kitalu. Kama mkulima, unapaswa kufanya chochote kinachowezekana ili kufanikiwa na biashara yako.
Faida ya kupanda mboga za majani katika banda kitalu ni kwamba unaweza kudhibiti hali ya hewa na joto. Magonjwa na wadudu wanaweza pia kudhibitiwa. Mmea wa nyanya huhitaji halijoto tofauti kulingana na hatua yake ya ukuaji ili uweze kuzoea mazingira ya banda kitalu na kudhibiti wadudu na magonjwa.
Aina za nyanya
Kuna aina mbili za nyanya zinazopandwa kwenye banda kitalu: aina fupi (determinate) na aina ndefu (un determinate). Aina fupi ni nyana ambazo hutoa maua na kupandwa mara moja tu. Aina ndefu ni zile nyanya ambazo huendelea kutoa maua, na zinaweza kuvunwa mfululizo kwa muda mrefu.
Wakulima wanashauriwa kupata aina sahihi zinazofaa kupandwa kwenye banda kitalu ili kuokoa kwa wakati na pesa. Tofautisha aina za nyanya ambazo hupandwa shambani na zile ambazo hupandwa kwenye banda kitalu.
Kudhibiti wadudu
Wadudu hudhibitiwa kwa kutumia mitego, na kunyunyizia viuatilifu kwenye banda kitalu. Panda miche kwenye viriba vikubwa ili kupunguza ushindani wa virutubisho.
Udongo uliochanganywa na mbolea hutumika ili kutolea mimea virutubisho katika viwango vilivyosawazishwa. Udongo huo huchanganywa na kalsiamu nitrati na kujazwa kwenye viriba. Mbegu hupandwa sm 1 au 2 chini ya udongo ili kurahisisha uotaji. Mbegu huota siku 7–10 baada ya kupandwa, na kisha hunyunyizwa na mmumunyo wa mbolea.
Kupandikiza
Kabla ya kupandikiza, safisha banda kitalu ili kuhakikisha kuwa mazingira hayana wadudu wala magonjwa. Kisha mwagilia mimea maji na pia nyunyizia mbolea.
Umbali wa 40 cm kwa 60 cm huachwa kati ya mimea ili kutoa nafasi ya kutosha. Mmumunyo wa mbolea hutumiwa kutoa virutubisho kwa mimea. Tuima kiwango cha chini cha virutubisho wakati mimea ni michanga, na ongezeka kiwango mimea inapokua.