Kunyausha ni mchakato wa kuacha mmea shambani baada ya kukatwa ili uweze kukauka. Kisha mmea hukusanywa na hutumika kama malisho ya mifugo.
Baada ya kuvuna mimea, itandaze kwenye jua kwa masaa machache ili inyauke. Katakata na kuchanganya mimea iliyonyauka na malisho mengine kama vile mabua ya mahindi au nyasi ya napier, na kisha ulishe mifugo. Kwa siku, ng‘ombe anaweza kulisha hadi kilo 70 za malisho ambayo hayajakaushwa, na kilo 20 tu kwa malisho yaliyokaushwa. Kulisha mifugo malisho yenye unyevu husababisha uyabisi wa tumbo hasa kwa ndama. Mihogo pia inaweza kutumika kama malisho ya mifugo, kwani majani yake yana vitamini na protini kwa kiasi cha 16% –18%.
Kutumia mihogo
Unapotengeneza silaji unaweza kuchagua kuchanganya majani ya muhogo na silaji ya napier au silaji ya mahindi ili kuongeza viwango vya protini. Mbegu za muhogo hazitumiki.
Malisho ya muhogo ni bora kwa mbuzi wa maziwa kwani ni mbadala wa protini.
Malisho mengine zaidi
Calliandra calothyrsus inayojulikana kama mti wa calliandra ni kichaka cha malishe ambacho kinaweza kukuzwa, na hakina miiba. Pia kinaweza kutumika kama mbadala wa malisho ya kutoa maziwa. Ni rahisi kukuza na kutunza, hukua haraka, hustahimili udongo wenye tindikali, na husaidia kuongeza nitrojeni kwenye udongo.
Unapolisha wanyama, mtolee kila mnyama 2kg-4kg kwa siku. Thamani ya lishe ya mti hupungua kadri unavyochanua maua.
Faida za calliandra
Calliandra hutolea mbuzi protini nzuri, nishati na madini. Huongeza uzalishaji wa maziwa kwa mbuzi kutoka lita 1 –2 lita kwa siku. Calliandra huboresha rutuba ya udongo, na husaidia kudhibiti mmomonyoko wa udongo katika maeneo wazi.
Pia ni hutoa kuni kwani hukua haraka, na hutoa mkaa. Majani yanaweza kutumika kama matandazo shambani, na kama mbolea ya kijani kwani huongeza nitrojeni kwenye udongo.