Malisho ni chakula kinachotolewa kwa wanyama wa kufugwa kama vile ng‘ombe, sungura, kondoo, farasi, kuku na nguruwe.
Baadhi ya malisho ni pamoja na: nyasi, majani, silaji, kunde n.k. Wakulima wengi nchini Kenya hutumia malisho kulisha mifugo yao. Malisho hutofautiana kulingana na fumuele, ladha na lishe, na hivyo ni muhimu kusawazisha malisho ili kuwatolea wanyama madini yanayohitajika.
Aina za malisho
Kuna malisho kadhaa ambayo yanaweza kulishwa kwa wanyama na haya ni; nyasi ya Sudan, desmodium, lucern, mahindi mabichi, mtama, mikunde, majani ya viazi vitamu, nyasi ya kikuyu na nyasi nyota.
Desmodium ni malisho ya jamii ya kunde yenye protini na madini, lucern ni malisho yenye protini na nyasi. Malisho ya nafaka kama mtama, nyasi ya Sudan na mchanganyiko wa haya yote hutimiwa kutengeneza silaji.
Kupanda na kutunza malisho
Unapopanda nyasi ya napia, acha umbali wa futi 2 kwa futi 2 kati ya mimea. kwa desmodium, acha umbali wa futi 1 kwa futi 1. Kwa viazi vitamu, acha umbali wa sm 45 kwa sm 30 kati ya mimea
Ongeza mbolea ya NPK (Nitrojeni, Fosforasi na Potasiamu). Kwa kupanda malisho, wakulima wanaweza kupunguza gharama za uzalishaji, na hivyo kuongeza faida.
Kujumuisha malisho
Wakulima wanashauriwa kupanda aina mbili za malisho kwenye shamba. Hata hivyo, mimea itashindana kupata virutubisho kwa sababu, na hivyo tumia mbinu bora za usimamizi. Nyasi ya napia na desmodium hukatwa ili ziweze kukua upya na zinaweza kudumu takriban misimu 8–10 ambayo ni takriban miaka 4–5.
Ubora wa malisho ya mifugo huamuliwa na mambo kadhaa, ambayo ni pamoja na; madini kam vile protini, fumuele, n.k.
Soma zaidi kuhusu kilimo cha malisho ya ng‘ombe wa maziwa nchini Kenya -Sehemu ya 2