Mahindi yamekithiri wanga, protini na madini, na hutumiwa kama msingi wa wanga katika milo mbalimbali duniani kote.
Kuna wadudu na magonjwa kadhaa ambayo husababisha upungufu wa mavuno ya mahindi. Magonjwa ni pamoj na ukungu, ubwiri unga, madoa, kuoza kwa mizizi, bakajani, chule na wadudu waharibifu ni panzi, viwavi jeshi, mchwa nakadhalika. Magonjwa hayo husababishwa na bakteria, fangasi na virusi na yanaweza kudhibitiwa kwa kusafisha mashamba baada ya kuvuna, kubadilisha mazao, kupanda aina sugu na kudhibiti wadudu. Ili kudhibiti wadudu, nyunyiza na kemikali zinazopendekezwa, haribu vilima vya mchwa shambani.
Mbinu za kilimo
Unapopanda, weka kilo 200 za NPK kwa hekta kwa udongo wenye rutuba, na kilo 600 kwa udongo usio na rutuba. Mbolea huongezwa katika hatua mbili ambazo ni wakati wa kupanda na wiki 5 hadi 6 baadaye. Dhibiti magugu ili kupunguza ushindani wa virutubisho, na pia dhibiti wadudu na magonjwa.
Runda udongo kuzunguka mmea ili kufunika mizizi iliyo wazi. Palilia wiki 2 baada ya kupanda na weka mbolea kabla ya kupalilia mara ya pili yaani baada ya wiki 6 hadi 7.
Dhibiti wadudu na magonjwa kwa kuchagua aina sugu, na kutumia kemikali inayopendekezwa. Iwapo mkulima hana pesa, nyunyiza mimea kwa mchanganyiko wa maji na sabuni ambao hudhibiti viwavijeshi.
Baada ya kuvuna, changanya mabua ya mimea kwenye udongo ili kuongeza mboji na kuboresha rutuba na uzalishaji.