Nchini Kenya kilimo cha embe kinahusisha aina tofauti za maembe, na umagiliaji hufanywa kwa kutumia maji ya mto katika baadhi ya mashamba.
Hizi ni aina tofauti za maembe; maembe ya tufaha ambayo ni umbo la mduara, makubwa na ya manjano; Tommy ambayo ni mviringo, rangi nyekundu na kubwa sana; Kent ambalo ni kubwa na la kijani kibichi lakini ni tamu sana linapoiva na kwa kawaida huchukua muda mrefu kukua; embe hisia lina mwonekano mweusi lakini linapendwa na wadudu; na van dyke ambalo ni aina ya embe tamu na ghali zaidi. Aina inayojulikana zaidi ni embe la tufaha na embe refu linalojulikana kienyeji kama nyowe.
Kubebesha au kuunganisha miembe
Kuunganisha huwasaidia miembe kustahimili magonjwa, kukua vyema na kuondoa sifa duni, jambo ambalo kuboresha mavuno. Wakati mche umekua hadi futi moja, huo ndio wakati sahihi wa kuunganisha miembe.
Baada ya kuunganisha miembe, unaweza kuanza kupata maembe mara moja, lakini inashauriwa uanze kuchuna baada ya takriban miaka mitatu ili kupata maembe bora.
Kudhibiti wadudu
Wadudu na magonjwa kama vile ukungu, ubwiri unga, hushambulia matunda machanga, maua na majani, na kuyaacha yakiwa yamefunikwa na unga mweupe na mara nyingi kupata vidonda. Kya hivyo, tumia dawa ya ukungu kwenye sehemu zinazoshambuliwa kwa matibabu bora. Mafuta ya mwarobaini yanaweza pia kutumika kama kinga.
Nzi wa maembe hunaswa na chambo. Kuna chambo cha majimaji kinachovutia inzi jike na chambo kigumu kinachovutia wadudu dume. Iwapo kuna ugonjwa wa kutu ya majani, tumia kiuatilifu.
Masharti bora
Miembe hustawi kwenye udongo wa kichanga ulio na mboji, usiotwamisha maji maji na pH ya 6–7. Pia hali bora ya hewa ilio na mvua, pamoja na msimu ya kiangazi wa miezi 4–5 ni nzuri kwa kilimo cha miembe. Mwanga wa kutosha pia ni muhimu kwa uotaji na kuchipuka, kwa hivyo kukata matawi ni muhimu.