Kuna aina mbili za kahawa ambazo ni; arabica na robusta. Kahawa ya Arabica hupandwa katika maeneo ya nyanda za juu huku robusta ikipandwa katika maeneo ya nyanda za chini.
Kahawa hufanya vizuri kwenye udongo wenye kina kirefu, usio na maji mengi sana, na wenye rutuba. Miti au migomba inaweza kupandwa pamoja na kahawa ili kutolea mikahawa kivuli. Ni muhimu kuondoa magugu kwa kunyunyizia dawa au ku’ongo. Miche yenye dalili za njano, dhaifu na shina ndogo inapaswa kukataliwa. Chimba mashimo na panda kahawa huku ukisimika vigingi vya kuimarisha mmea. Wadudu na magonjwa yanayoathiri kahawa ni funza mweusi, kutepeta, mnyauko, madoa ya kahwia n.k. Ng‘oa sehemu zote zilizoathirika na uzichome moto.
Muachano kati ya mikahawa
Kwa kahawa ya robusta, tumia muachano wa futi 10 kwa 10 ili kupata mikahawa 450 katika ekari moja. Kwa kahawa ya arabica, tumia muachano wa futi 8 kwa 8 ili kukupa mikahawa 680 katika ekari moja.
Chimba mashimo yenye upana wa futi 2 na kina cha futi 2 na weka udongo wa juu kwenye upande wa juu wa shimo, na udongo chini kwenye upande wa chini wa shimo angalau miezi 3 kabla ya kupanda. Jaza shimo kwa udongo wa juu uliochanganywa na samadi.
Kupanda kahawa
Mwagilia miche maji kabla na baada ya kupanda. Baada ya miezi sita, pinda mimea kuelekea machweo ili kuchochea ukuaji wa machipukizi. Acha tu machipukizi 2–3 yenye afya kutoka na upogoe mengine.
Pogoa kahawa ifikapo miaka 7–9, kata tawi moja futi 1 kutoka ardhini kila mwaka. Kata tawi kwa pembe inayoinama ili kuzuia maji kukusanyika, jambo ambalo linaweza kusababisha kuoza.
Kuvuna na kushughulikia kahawa baada ya kuvuna
Vuna buni za kahawa zilizoiva tu. Safisha buni za kijani kibichi ndani ya masaa 12 baada ya kuvuna, na uziweke kwenye chombo kwa masaa 12–24 ili kuruhusu uchachushaji. Osha mbuni za kahawa zilizochacha kisha uyakaushe kwenye wavu. Katika usindikaji kavu, unaweza kukaushia mbuni za kahawa juu ya sakafu ya saruji.
Uhifadhi hufanywa katika magunia na mbuni za kahawa huwekwa kwenye jukuwa lililoinuliwa angalau 0.5 ft juu ya ardhi ili kuzuia unyevu kuingia.