Tutaangalia kilimo cha chai nchini Kenya, mambo yanayoathiri kilimo cha chai nchini Kenya na maeneo ambayo chai hukuzwa nchini Kenya.
Chai hukuzwa kwa kiwango kidogo na kikubwa nchini Kenya. Hulimwa zaidi na wakulima wadogo nchini Kenya. Chai ni zao linaloongoza kwa kulimwa nchini Kenya kumaanisha kuwa linaiingizia taifa fedha nyingi za kigeni. Ni zao ambalo linahitaji kazi kubwa wakati wa kuvuna.Chai inahitaji udongo wa volkeno usio na maji na ambao una asidi kidogo. Hatimaye chai inahitaji kazi kubwa hasa wakati wa kuvuna.
Sababu za kukua chai
Ili chai iweze kuishi, inahitaji mambo fulani. Inahitaji mwinuko wa juu kumaanisha inalimwa hasa katika nyanda za juu za Kenya.
Chai ni zao ambalo linahitaji hali ya hewa ya baridi na halijoto ya nyuzi joto 20 hivi. Chai inahitaji udongo wa volkeno usio na maji na ambao una asidi kidogo. Hatimaye chai inahitaji kazi kubwa hasa wakati wa kuvuna.
Maeneo ya kukua
Maeneo haya yamegawanyika katika sehemu mbili; maeneo ambayo chai hukuzwa kwa kiwango kikubwa kwa mfano, Kericho, Murang‘a, Meru, Sotik, na Bomet.
Pia tuna maeneo ambayo chai hukuzwa kwa kiwango kidogo kwa mfano, Vihiga, Nyeri, Maragua na Gucha.
Umuhimu wa chai
Chai ni zao la biashara linalolimwa kwa manufaa yake sisi binadamu na pia kwa uchumi wetu kama nchi. Ni chanzo cha ajira.
Chai inaiingizia nchi fedha za kigeni kupitia mauzo ya nje. Chai pia imesababisha maendeleo ya miundombinu hasa katika maeneo ambayo chai inalimwa tumejenga barabara za kuwezesha usafiri.