»Kiini changu cha kwanza – Kipindi cha 3 – Wakati sahihi wa Kuweka kitenga malkia katika mzinga«
Unapomtambua nyuki-malkia na kugundua kuwa kila fremu ina kitu ndani yake, angalia iwapo kuna magonjwa ndani ya mzinga kabla ya kuweka kitenga malkia.
Kisha jiandae kwa kuvaa vazi maalu la kushughulikia nyuki. Tumia kifaa cha kutoa moshi ili kuondoa nyuki kabla ya kushughulikia ndani ya mzinga. Hakikisha kuwa halijoto halipo chini ya nyuzi joto 13 au 14 wakati unaposhughulikia mzinga. Pia, hakikisha kwamba unafanya ukaguzi wa mzinga kila wiki.
Kuweka kitenga malkia
Jambo la kwanza unalotaka kuona kwenye bustani yako ya nyuki ni idadi kubwa ya nyuki vibarua ambapo takriban asilimia 80 ya fremu za mizinga iwe imefunikwa na nyuki.
Katika mzinga wa unene wa fremu 10, unapogundua kuwa nyuki wamefunika takriban fremu 9 kwa wiki moja, ndipo hapo unapaswa kuweke kitenga malkia. Unapoweka kitenga malkia, hakikisha kuwa nyuki wote wameondolea kutoka juu ya fremu.
Udumishaji
Angalia fremu za mzinga moja baada ya nyingine ili kuona maendeleo yalipo kama vile uwepo wa mayai.
Iwapo haujaona ugonjwa wowote wakati anapokagua mzinga, basi weka kitenga malkia na pia ongeza juu yake kisanduku ambacho husaidia kuhifadhi asali ya ziada.
Tolea nyuki wako chakula cha kutosha. Kisha funika mzinga ipaswavyo.