Uhimilishaji Bandia (AI) ni mchakato ambao shahawa (mbegu) huwekwa ndani ya mfumo wa uzazi wa mnyama jike ili atunge mimba.
AI husaidia kueneza shahawa kutoka kwa dume aliye na sifa bora na kuzuia kuenea kwa magonjwa yanayonezwa wakati dume akimpanda jike. Kuna vifaa kadhaa vinavyohitajika kama vile mtungi wa kuhifadhia mbegu ambao huwekewa hewa ya nitrojeni, mrija wa shahawa iliyogandishwa, bomba la kukusanya shahawa, mkasi, kipimajoto, maji ya vuguvugu. Hakikisha hakuna pengo kati ya mkato wa mrija wa shahawa na nailoni ili kuzuia sehemu ya shahawa isibaki kwenye mrija. Uke wa mnyama unapaswa kutambuliwa na mtu aliye na ujuzi juu ya uzazi.
Hatua za kufuata
Anza kwa kutambua nambari ya dume kutoka kwa lebo iliyoambatanishwa kwenye mtungi. Kisha inua chombo kilicho ndani ya mtungi hadi kitakapofika shingoni mwa mtungi. Chukua mrija wa shahawa ukitumia kibano kwa haraka iwezekanavyo na uziunde ili kuondoa nitrojeni ya ziada.
Zingatia hali joto sahihi na wakati unapoweka mrija wa shahawa kwenye maji ya joto ili kufikia kiwango cha juu cha uponaji wa shahawa.
Baada ya kuyeyusha, futa mrija wa shahawa kwa upole ili kuondoa maji.
Kisha weka karatasi ya nailoni juu ya kifaa cha kuingiza shahawa na uimarishe na pete. Hakikisha umevaa glavu za kujikinga ili kuepuka maambukizi, tumia vilainishi na upanue vizuri mfumo wa uzazi.
Fungua mlango wa uke na ingiza kifaa cha kuingiza shahawa kwa pembe ya 30– 40 ili kuepuka ufunguzi wa tundu la mkojo. Chomeka kifaa cha kuingiza shahawa kwa upole hadi kitakapofika kwenye kuta za ndani za tumbo la uzazi.
Baada ya kutenda mchakato wa AI, kanda kwa upole kisimi mara kumi ili kupata matokeo mazuri. Mwisho, uhimilishaji bandia unafaa kufanywa katika nyakati zinazofaa ili kupata kiwango cha juu cha utungaji mimba.