Usimamizi bora wa shamba la mikahawa, huongeza mazao. Kukausha kahawa vizuri na kuhifadhi ni mambo makuu ya kudumisha ubora na kuongeza mapato kutoka kwa kahawa.
Mbinu bora za usimamizi wa kahawa huongeza mapato. Kuchuna, usimamizi bora na uhifadhi husababisha mapato.
Kuchuma kahawa
Chuma tu mbegu ziliyoiva angalau mara moja kwa wiki. Epuka kuvuna mbegu kiholela, kwa sababu utavuna mbegu ambazo hazijaiva pamoja na Kuacha kovu ambapo ugonjwa unaweza kuingilia kwa urahisi. Pia usiruhusu mbegu kuiva sana kwa sababu hufanya huku hupunguza ubora wa mbegu. Vuna mbegu zote mwishoni mwa msimu ili kuzuia kuenezwa kwa wadudu na magonjwa. Pia, tumia turubai safi na vyombo safi vya kuvunia.
Kukausha kahawa
Kausha mbegu kwenye turubai au damani ya plastiki kwa sababu ardhi wazi huathiri ubora wa mbuni pamoja na kuhimiza ukuaji wa ukungu. Tandaza mbegu za kahawa kwa angalau mita 3 na endelea kuzipindua ili zikauke sawasawa. Hifadhi mbuni za kahawa zikiwa zimekauka kwa kuzileta chumbani ikiwa kuna uwezekano wa mvua kunyesha. Unaweza pia kuzifunga kwenye maturubai wakati kuna uwezekano wa mvua. Kausha mbuni za kahawa kwa siku 5 – 8 ili kudumisha ubora. Pima kiwango cha unyevu ukitumia kipimaji cha unyevu, kuziuma kwa meno, kutumia sauti ya mbegu zinapotikiswa, au kukata mbuni katika vipande viwili. Daima hifadhi mbuni kwenye gunia safi, kwenye mahali palipoinuka pamoja na mzunguko bora wa hewa. Pia, mbuni hazifai kuwa karibu na kuta ili kuepuka unyevu kuzingia.