»Jinsi ya kutumia hatua nzuri za usalama shambani«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=cnGumh45VPE

Muda: 

00:06:16
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

ADM Animal Nutrition Vietnam

Usalama shambani unahusisha mbinu zote zinazotumika kabla na wakati wa kufuga wanyama ili kuboresha hali za ufugaji na kupunguza uwepo wa vimelea vya magonjwa.

Mlipuko wa magonjwa shambani huathiri matokeo ya kitaalam na kiuchumi. Hata hivyo, magonjwa haya yanaweza kudhibitiwa kwa ufanisi kwa kutekeleza hatua za usalama. Unapotumia viuatilifu, hakikisha kwamba unatumia dawa zenye ufanisi ili kuua vimelea vya magonjwa.

Hatua za usalama

Punguza uwasiliano kati ya wanyama wa kufugwa na wanyama porini kwa kuweka uzio kuzunguka shamba.

Pia dhibiti ufikiaji wa watu shambani, na hakikisha unaosha na kuua viini kwenye magari yanayoingia shambani ili kuzuia uchafuzi kutoka kwa vimelea vya nje.

Watu wanaoingia shambani wanapaswa kuoga na kuvaa nguo safi. Tenganisha wanyama wapya walionunuliwa kwa mwezi mmoja ili kuepuka kueneza vimelea vya magonjwa.

Tumia uhimilishaji bandia, na angalia shamba lilitolewa shahawa ili kudhibiti kuenea kwa magonjwa ya sehemu za uzazi.

Pia ni muhimu kutenganisha wanyama kulingana na umri ili kuongeza upinzani kwa magonjwa.

Hakikisha unasafisha na kukausha banda ili kuondoa kuua vimelea vya magonjwa. Baada ya kusafisha, usitumie banda kufuga wanyama wapya kwa siku 7.

Hakikisha kwamba vifaa vinavyotumiwa lazima vimesafishwa. Weka nyavu kwenye banda ili kuzuia ndege wa porini wanaobeba vimelea vya magonjwa.

Pia tekeleza mpango wa kudhibiti na kuondoa wadudu kwenye eneo, na usitumie mabaki ya jikoni bali tumia malisho kutoka kwa muuzaji anayeaminika.

Tia dawa kwenye maji ya kunywa ya wanyama, safisha mfumo wa usambazaji wa maji ili kuondoa vimelea vya magonjwa.

Hakikisha unachanja mifugo ili kuongeza kinga za wanyama dhidi ya virusi, tenganisha wanyama wagonjwa ili watibiwe ipaswavyo. Choma wanyama waliokufa, tibu samadi ili kuua vimelea vya magonjwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:36Magonjwa ya mifugo huathiri matokeo ya kitaalam na kiuchumi. Magonjwa haya yanaweza kudhibitiwa kwa ufanisi kwa kutekeleza hatua za usalama.
00:3701:07Punguza uwasiliano kati ya wanyama wa kufugwa na wanyama porini.
01:0801:28Osha na kuua viini kwenye magari yanayoingia shambani
01:2902:10Watu wanaoingia shambani wanapaswa kuoga na kuvaa nguo safi. Tenganisha wanyama wapya walionunuliwa kwa mwezi mmoja
02:1102:38Tumia uhimilishaji bandia
02:3903:14Tenganisha wanyama kulingana na umri
03:1503:37Hakikisha unasafisha na kukausha banda la mifugo. Usitumie banda kufuga wanyama wapya kwa siku 7.
03:3804:01Safisha banda na vifaa vya shambani mara kwa mara.
04:0204:31Weka nyavu kwenye banda ili kuzuia ndege wa porini wanaobeba vimelea vya magonjwa. Tumia malisho kutoka kwa muuzaji anayeaminika lakini sio taka za jikoni.
04:3205:02Tia dawa kwenye maji ya kunywa ya wanyama, safisha mfumo wa usambazaji wa maji na chanja mifugo
05:0306:16Tenganisha wanyama wagonjwa ili watibiwe ipaswavyo. Choma wanyama waliokufa, tibu samadi ili kuua vimelea.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *