Wakati wa misimu ya kilele, ndizi huwa nyingi. Kwa hivoyo, nyingi huharibika na kutupwa kama taka. Walakini, hizi hizo zinaweza kutumika kutengeneza mbolea bora ya maji.
Utengenezaji wa mbolea ya maji
Ili kutengeneza mbolea kutoka kwa ndizi, unahitaji kupata ndizi zilizoiva na uzikate katika vipande vidogo. Baada ya kukata ndizi, tumia blenda kutengenza mchanganyiko. Mimina mchanganyiko kwenye chombo na kisha ongeza maji ndani yake.
Funga chombo na ukiweke mahali pa baridi.
Subiri kwa siku 7 na baada ya hapo, mchanganyiko utajitenga kwa safu 2. safu 1 imeganda huku nyingine ni ya maji. Changanya safu mbili hizo vizuri, na kisha mimina mchanganyiko kwenye ndoo yenye lita 5 za maji.
Huu ni mchanganyiko tayari kutumika kama mbolea na hunyunyizwa kwenye eneo la mizizi ya mimea.