»Jinsi ya Kutambua na kukagua viwavijeshi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://sawbo-animations.org/708

Muda: 

00:06:08
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

SWABO

Viwavijeshi ni wadudu waharibifu wa mimea ya mahindi na husababisha uharibifu mkubwa wa mazao. Hata hivyo, mbinu jumuishi za usimamizi hupunguza uvamizi wao.

Kukagua mahindi, kudhibiti viwavi mapema pamoja na kutumia viuatilifu visivyoharibu mazingira ni baadhi ya hatua bora zinazosababisha mavuno mengi na mapato ya ziada. Mabuu ni hatua ya uharibifu zaidi, hata hivyo usikague shamba baada ya kunyunyizia viuatilifu kwani vinaweza kuathiri afya yako. Epuka safu zilizo ukingoni mwa shamba iwapo unachagua maeneo ya uchunguzi.

Kukagua viwavijeshi

Tafuta uharibifu wa majani kama vile mashimo madogo, kinyesi cha viwavi, na mashimo kwenye gunzi la mahindi.

Kagua shamba ukifuata muundo wa herufi W, kwanzia mita 5 kutoka ukingoni mwa shamba. Fanya uchunguzi mapema wakati majani ya mahindi yanajifunua. Kagua kila mmoja ya maeneo 5 yaliyochaguliwa.

Katika kila mmoja ya maeneo haya 5, angalia kati ya mimea 10 hadi 20 kwa dalili za uharibifu wa viwavijeshi. Rekodi idadi ya mimea iliyoangaliwa na mimea iliyoharibiwa.

Wakati mimea inapojifunua majani ya kwanza, unafaa kurekodi miche iliyoharibiwa. Wakati mimea imejifunua majani yote, chunguza majani 2– 4 mapya kujitokeza.

Rekodi mimea iliyoharibiwa kwa kila mimea 10 – 20 katika kila eneo. Iwapo angalau mimea 4 kati ya mimea 10 imeharibiwa, shauriana na mtalamu wa kilimo kuona kama thamani ya zao itazidi gharama ya ulinzi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:30Viwavijeshi ni wadudu waharibifu wa mimea ya mahindi. Maisha ya viwavijeshi.
00:3100:41mbinu jumuishi za usimamizi wa wadudu
00:4200:57Kukagua mahindi, kudhibiti viwavi mapema pamoja na kutumia viuatilifu visivyohatari
00:5801:13Kukagua viwavijeshi
01:1401:45Tafuta uharibifu wa majani uliosababishwa na viwavijeshi
01:4601:57Tafuta kinyesi cha viwavi, na uwepo wa viwavi vikubwa
01:5802:08Tafuta mashimo kwenye gunzi la mahindi.
02:0902:47Kagua shamba mapema. usikague shamba baada ya kunyunyizia viuatilifu
02:4803:13Kagua shamba ukifuata muundo wa herufi W, kwanzia mita 5 kutoka ukingoni mwa shamba.
03:1403:25Epuka safu zilizo ukingoni mwa shamba. Angalia kati ya mimea 10 hadi 20 na katika kila moja ya maeneo 5
03:2603:38Sajili mimea iliyokaguliwa, na iliyoharibiwa.
03:3904:02Wakati mimea inapojifunua majani ya kwanza, unafaa kurekodi miche iliyoharibiwa.
04:0304:18Wakati mimea imejifunua majani yote, chunguza majani 2– 4 mapya kujitokeza.
04:1904:41Rekodi mimea iliyoharibiwa kwa kila mimea 10 -20 katika kila eneo. Shauriana na mtalamu wa kilimo.
04:4206:08Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *